Joshua Mqubuko Nyongolo Nkomo (19 Juni 1917[1]1 Julai 1999) alikuwa mwanasiasa, kiongozi na mwanzilishi wa chama cha Zimbabwe African People’s Union (ZANU) na pia ni mtu wa kabila la Kalanga[2] kutoka nchini Zimbabwe. Huyu alikuwa anajulikana kama baba wa Zimbabwe au katika Lugha ya Zimbabwe ‘’umdala Wethu, Umafukufuku au chibwechitedza’’ jiwe linaloteleza au (the slipery rork)

Joshua Nkomo.

Maisha ya awali

hariri

Nkomo alizaliwa katika sehemu ya Somokwe katika ardhi ya Matebele mwaka 1917, katika familia ya watoto nane. Baba yake alikuwa anaitwa Thomas Nyongolo Letswansto Nkomo, aliokuwa akifanya kazi kama mchungaji na pia alikuwa ni mfanyakazi katika Chama cha Kimishonari cha London au London Missionary Society.

Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi katika jimbo la Rhodeshia alijifunza masomo ya ufundi useremala katika shule ya Viwanda ya Tsholotso ambapo alisoma hapo kwa muda wa mwaka mmoja na baadae akawa dereva.

Baadae alifanya kazi kama mfugaji na baadae akawa mwalimu na alikuwa mahususi katika maswala ya useremala katika shule ya Manyame katika jimbo la Kezi.

Mwaka 1942, akiwa na miaka 25, na bado akiwa na kazi yake kama mwalimu, aliamua kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo na hatimaye kuwa fundi seremala mahususi.

Alijiunga na chuo cha Adams na Chuo cha Ufundi cha Jan Hofmeyer nchini Afrika ya Kusini. Akiwa hapo alikutana na Nelson Mandela na viongozi wengine mbalimbali waliokuwa katika chuo kukuu cha Fort Hare University of Fort Hare japokuwa hakuwa akisoma katika chuo kikuu hicho. Ni katika chuo cha ufundi cha Hofmeyr.Hofmeyr School of Social Work ambapo ndipo alipopata shahada yake ya kwanza katika masuala ya Sayansi ya Jamii mwaka 1952.

Nkomo alimuoa Johanna Mafuyana tarehe 01/10/1949.

Baada ya kurudi kutoka Bulawayo mwaka 1947, alikuwa kati ya wapigania haki wafanyakazi wa shirika la Reli na Baadae kuwa kiongozi wa Umoja wa wafanyakazi wa Reli na baadae kuwa kiogozi wa African National Congress mwaka 1952. Mwaka 1960, alikuwa raisi wa chama cha National Democratic Part ambacho baadae kilifungiwa na serikali ya Rhodesia. Pia Nkomo amekuwa ni moja kati ya wajasiriamali matajiri zaidi katika eneo la Rhodesia.

Mapinduzi ya Silaha

hariri

Nkomo alitiwa Kizuizini katika kambi ya Gonakudzingwa na serikali ya Ian Smith mwaka 1964, wanamapinduzi wenzake kamam vile Ndabaningi Sithole, Edger Tekere Maurice Nyagubo na Robert Mugabe hadi mwaka 1974, lakini baadae waliachiwa baada ya shinikizo kutoka na Raisi wa Afrika ya Kusini.during the apartheid eraSouth African B.J.Vorster. Baada ya Kuachiwa, Nkomo alienda nchini Zambia kuendelea na mapambano ya chini chini na pia majadiliano. Tofauti na ZANU yaani (Zimbabwe African National Liberation Army) na mapambano ya silaha , chama cha ZAPU (Zimbabwe people’s Revolution Army) kilikuwa kimeamua kufanya mapambano ya msituni na mazungumzo. Katika kipindi cha uhuru, ZIPRA ilikuwa na silaha za kijeshi za kisasa na zilizokuwa zimehifadhiwa katika nchi za Zambia na Angola iliyokuwa pamoja na silaha nyingine za kivita kulikuwa na mizinga ya vita na wafanyakazi wa kisasa katika matumizi ya vifaa ivyo.

Jaribio la Kuuwawa

hariri

Joshua Nkomo alikusudiwa kufanyiwa mauaji mara mbili, mara ya kwanza ikiwa ni Nchini Zambia, lakini lengo hilo halikufanikiwa lakini pia lakini majaribio ya kumuua yalindelea na baadae yalifanywa na Rhodesia Special Air Service. Katika malengo hayo yalihusha nyumba aliyokuwa akiishi, kiongozi wa jaribio hilo alijaribu kuotroka lakini alikamatwa na mlinzi wa Nkomo akiwa amenaswa katika dirisha na bafuni. [3].

Majeshi ya ZAPU, yalifanya mambo mengi ya matumizi ya nguvu katika kuiondoa madarakani serikali ya Rhodesia. Moja kati ya mambo yanayasadikika kuwa ni ya kinyama zaidi kuwahi kutokea ni pamoja na mauaji katika ndege za abiria. Ya kwanza yalitokea tarehe 3/09/1978 na kuua watu 38, kati ya watu 56, na wengine kumi wakijeruhiwa, ikiwa ni oamoja na watoto. Waliobaki hai, walitembea kutoka kuotka eneo hilo hadi Kariba kiasi cha umbali wa kilometa 20.

Baadhi ya wasafiri walikuwa wamejeruhiwa vibaya, ,na baadhi alichukuliwa na polisi wa jeshi la Rhodesia, Jaribio la pili lilikuwa tarehe 12/02/1979 na kuua watu 59, papo hapo, lakini malengo ya shambulizi la pili yalikuwa kwa ajili ya Peter Walls mkuu wa COMOPS (Commander Combined Operations) aliyekuwa anahusika na vifaa maalumu kama vile. Special Air ServiceSAS Walls alipokea tiketi ya kuondoka na ndege ya pili kutokana na idadi kubwa ya watalii, ndege ambayo iliondoka Kariba dakika 15, baada ya ndege iliyopotea. Hakuna mtu aliyeshitakiwa kwa makosa ya ndege kupotea kutokana na kutolewa kwa msamaha kutoka kwa Smith na Mugabe.

Katika mahojiano ya Televisheni, muda mfupi baada ya kupotea kwa ndege nyingine, ambapo, akiwa anacheka Nkomo alitania kuhusiana na matukio hayo na kuhakikisha kuwa ZAPU ndio wanaohusika na mashambulizi ya ndege mbalimbali. Katika vitabu vyake mbalimbali kama vile ‘’Story of my Life’’ kilichochapishwa mwaka 1985, Joshua Nkomo ameelezea masikitiko yake kuhusiana na mashambulizi ya ndege zote mbili

 

Nkomo alianzisha chama cha National Democratic Part (NDP) , na mwaka ambao waziri Mkuu wa Uingereza bwana Harold Macmillan alipoongelea “upepo wa mabadiliko” unavuma katika Afrika Robert Mugabe aliungana nae. Chama cha NDP kilifungiwa na serikali ya kibabe ya Smith na baadae chama cha Zimbabwe African People Union ZAPU ambacho pia kilianzishwa na Joshua Nkomo pamoja na Robert Mugabe mwaka 1962, kilichua nafasi ya NDP. Lakini pia kilizuiwa mapema. Chama cha ZAPU, kiligawanyika mwaka 1963, wakati wengine walihisi mgawanyiko huo ulikuwa ni kutokana na masuala ya Kikabila, lakini zaidi inaonesha kuwa mgawanyiko huo ulitokana na kushindwa kwa Sithole, Mugabe, Takawira na Malianga kuchukua madaraka ya ZAPU kutoka kwa Nkomo. ZAPU kikabaki chama chenye mjumuisho wa makabila mengi hadi kupatika kwa uhuru.

Serikali ambayo haikwa maarufu ilioyitwa Zimbabwe-Rhodesia ilioyokuwa inaongozwa na Abel Muzorewa iliundwa mwaka 1979kati ya Ian Smith na Ndabaningi Sithole’s. ZANU ambayo kwa wakati huo, ilikuwa tayari imeshagawanyika kutokana na Mambo ya kijeshi ya Mugabe. Lakini vita ilioyanzishwa na Nkomo na Mugabe viliendelea bila kupiganwa. Na Uingereza pamoja na Marekani havikuweka vikwazo katika nchi hiyo Uingereza ulivishawishi vyama hivyo kwenda katika Lancaster House mwezi wa tisa mwaka 1979, kwa ajili ya kuanzisha katiba na kuitisha uchaguzi upya. Mugabe na Nkomo walifanya makubaliano yaliyoitwa Patriotic Front (PF) katika makubaliano yaliyoendeshwa na Lord Carrington. Uchaguzi ulifanyika mwaka 1980, na katika macho ya wengi chama cha ZAPU kilichokuwa kinaongozwa na Nkomo kilishindwa katika uchaguzi huo na chama cha ZANU kilichoongozwa na Mugabe Matokeo ya uchaguzi huo. Yaliweka vyama vyote viwili ZAPU na ZANU katika vyama vinavyoegamia mfumo wa kikabila , yaani chama cha ZANU kikiwa na iadi kubwa ya ya kabila la Shona na chama cha ZAPU kikiwa na idadi kubwa ya kabila la Ndebele Nkomo alikaribishwa katika sherehe ya uraisi lakini alikataa.

Mapinduzi ya kijeshi

hariri

Hata baada ya kufikia lengo la kumwondoa Ian Smith na idadi kubwa ya wazungu.. bado Nkomo na Mugabe hawakuelewana. Nkomo alikuwa akijitahidi kuweka mahusiano mazuri katika vyama vyao viwili lakini Mugabe hakuwahi kuonesha ushirikiano kwani aliamini kuwa ZAPU kilikuwa na malengo ya kufanya mapinduzi na kukitoa madarakani chama cha ZANU. Wakati Julius Nyerere alipoviita vyama hivyo viwili katika mkutano uliokusudia kurejesha mahusiano mazuri, vyama hivyo viliingia katika ofisi ya Nyerere tafauti tofauti. Kwanza alianza Nkomo na kufuatiwa na Mugabe. Wakati Mugabe alipopewa kiti kwa ajili ya kukaa alimwambia Nyerere. "If you think I'm going to sit right where that fat bastard just sat, you'll have to think again" yaani “ kama unadhani naweza kukaa hapa na huyo mpumbavu alieakaa hapo, inabidi ufikirie tena” Kutoka na hali hiyo, mkazo uliongezwa kati ya mahusiano yao, mapigano kati ya chama cha ZANLA na ZIPRA yaliongezeka na kuongeza kutoelewana kati ya hawa watu wawili Hatimaye, baada ya majadiliano ya muda mrefu na kukataliwa mara kadhaa, Nkomo hatimaye alichaguliwa katika baraza la mawaziri, lakini mwaka 1982, alishtakiwa kwa kosa la kupanga mapinduzi ya kijeshi, baada ya mawakili kutoka Afrika ya Kusini kwenda Zimbabwe central Intelligence Organisation, kujaribu kutengeneza kutokuaminiana kati ya vyama vya ZAPU na chama cha ZANU, waliweka kwa kukusudia silaha katika mashamba yanayomilikwa na chama cha ZAPU na kwenda kutoa taarifa kwa Mugabe juu ya kukutwa kwa silaha katika katika mashamba hayo Katika hotuba yake, Mugabe alisema “ZAPU and its leader Dr. Joshua Nkomo, are like a cobra in a house the only way to deal with effectively with a snake is to strike and destroy its head ” yaani “ZAPU na kiongozi wake, Dr Joshua Nkomo ni kama nyoka ndani ya nyumba, njia pekee ya kufanya kwa nyoka na kumshambulia na kuharibu kichwa chake” Aliagiza kikosi cha jeshi kwa eneo analokaa Nkomo, yaani katika ardhi ya Matebele katika oparesheni ya Gukurahundi na kuua wandebele 3,000 katika jaribio la kutokomeza chama cha ZAPU na kutengeneza serikali chini ya chama kimoja. Nkomo alitoroka Nchini Zimbabwe, na Serkali ya Mugabe ikadai kuwa ametoroka akiwa amevaa kama mwanamke.

NKOMO KATOROKA: Kiongozi wa chama cha ZAPU, emetoroka kwenda katika maficho aliyojipa mwenyewe jijini London baada ya ya kutoroka bila kufuata sheria kupitia Botswana akiwa amevalia kama mwanamke tarehe07/03/1983, akidai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini na kuwa alikiwa akienda kutafuta masuluhisho ya Zimbabwe nje ya nchi (chapa ya serikali, Harare 1984) )[4].

Nkomo alidharau madai kuwa, alitoroka akiwa amevalia kama mwanamke, na kusema kuwa "I expected they would invent stupid stories about my flight..... People will believe anything if they believe that ". [4] He added that "...nothing in my life had prepared me for persecution at the hands of a government led by black Africans."[4]

Yaani, “ nilitegemea kuwa wataibua habari za kipumbavu juu ya kuondoka kwangu.,… watu wataamini chochote kama wameamini hayo” na kuongeza kuwa “hakuna kitu katika maisha yangu kilichoandakiwa kwa ajili ya kushtakiwa katika mikono ya serikali ya waafrika weusi. Baada ya amuaji ya kinyama katika Gukurahundi ya mwaka 1987, Nkomo hatimaye akakubali chama cha ZAPU kuingia katika chama cha ZANU, na kusababisha kuotkea kwa chama cha ZANU-PF na kuiacha nchi ya Zimbabwe kama nchi iliyo katika mfumo wa chama kimoja. Jambo lililosababisha baadhi ya watu wa kabila la Ndebele kumlaumu Nkomo kwa kuwauza kwa chama cha kigine. Lakini idadi ya watu wa kabila la Ndebele, walikuwa wachache kiasi cha kushindwa kutoa pingamizi lenye nguvuwakati wa kuunganishwa kwa vyama hivyo viwili. Katika hali ya kutokuwa na nguvu, na afya yake kuzidi kudorora hata ushawishi wake ukashindwa kuwa na mshiko na hivyo kufa Alipoulizwa katika maisha yake, kuwa kwa nini aliruhusu haya yote yatokee, alimwambia mwana historia kuwa Eliaki Sibanda kuwa, alifanya hivyo ili kusitisha mauaji ya watu wa kabila la Ndebele (ambao walikuwa wakiunga mkono chama chake) na ya wanasiasa wa chama cha ZAPU na wanaharakati ambao walikuwa wakilengwa na vyombo vya usalama vya Zimbabwe tangu mwaka 1982, alisema “Mugabe and his Shona henchmen have always sought the extermination of the Ndebele," yaani “Mugabe na Washona wake walitaka kufanya ukatili kwa Wandebele” alisema Nkomo amekuwa si muumini mzuri wa kanisa la kimeshenari katika sehemu kubwa ya maisha yake, alibadilisha dini na kuwa Mkatoliki Roman Catholicism mwaka 1999, muda mfupi baada ya kufariki kwa saratani ya kibofu yaani prostate cancer tarehe 01/07/1999 akiwa na umri wa mika 82, katika hospitali ya Parirenyatwa katika jimbo la Harare

Barua za Nkomo

hariri

Madai ya kuandikwa kwa barua na Nkomo kwenda kwa waziri mkuu Robert Mugabe akiwa uhamishoni, Uingereza yalianza kuibuka baada ya kifo chake mwaka 1999. katika barua zake , alilalamika kuhusu mateso yake na kuilamu serikali ya Zimbabwe kwa kutokomeza vyama vya upinzani. .[5]

Hadhi ya shujaa wa taifa

hariri

Mwaka 1999, Nkomo alitangazwa kuwa shujaa, na alizikwa katika makaburi ya mashujaa ya taifa Natioanal Heroes Acre katika jimbo la Harare.

Tarehe 27/06/2000, seti ya stampu nne zilitolewa na shirika na pasta na mawasiliano la Zimbabwe na kuonesha Joshua Nkomo. Zenye kuonesha badili la fedha ya ZW$2.00, $9.10, $12.00 and $16.00 ya yalikusudiwa na Cedric D Herbert.

Tanbihi

hariri
  1. Jessup, John E. An Encyclopedic Dictionary of Conflict and Conflict Resolution, 1945-1996. Page 533.
  2. Hill, Geoff. The Battle for Zimbabwe: The Final Countdown, 2003. Page 52.
  3. Cline, Lawrence E. (2005) Pseudo Operations and Counterinsurgency: Lessons from other countries, Strategic Studies Institute, p.11
  4. 4.0 4.1 4.2 Joshua Nkomo, The Story of My Life, Methuen London 1984 or Sapes books Harare 2001, p.1-4 "clown Herbert Ushewokunze, minister of home affairs"
  5. [1] Ilihifadhiwa 28 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. Zimbabwe Metro

Marejeo

hariri
  • Nkomo: The Story of My Life, Joshua Nkomo, Nicholas Harman (Author); 1984; ISBN 0413545008,ISBN 978-0413545008, Autobiography
  • The Zimbabwe African People's Union 1961-1987: A Political History of Insurgency in Southern Rhodesia.
  • Terence O. Ranger, ‘Nkomo, Joshua Mqabuko Nyongolo (1917–1999), Oxford Dictionary of National Biography, Oxford University Press, 2004 accessed 18 June 2006