Mapacha au ndugu pacha ni watu au wanyama waliozaliwa kwa pamoja kutoka tumboni mwa mama yao[1]. Kwa binadamu mara nyingi huwa wawili.

Marian na Vivian Brown, dada pacha wanaofanana.

Kuna aina kuu mbili za mapacha ambao ni wale wanaofanana na wale wasiofanana. Tofauti ni kwamba wa kwanza wametokana na kijiyai kimoja kilichofikiwa na mbegu moja, kumbe wa pili wametokana na vijiyai viwili vilivyofikiwa na mbegu mbili. Hivyo wa kwanza wana jinsia ileile na kwa kawaida kabisa DNA ileile, kumbe wa pili DNA zao ni tofauti, ila zinafanana kiasi kama zile za ndugu wote wenye baba mmoja na mama mmoja[2].

Kimataifa aina ya kwanza inatokea mara 3 katika ujauzito wa wanawake 1,000[3].

Tanbihi

hariri
  1. MedicineNet > Definition of Twin Ilihifadhiwa 22 Oktoba 2013 kwenye Wayback Machine. Last Editorial Review: 19 June 2000
  2. Michael R. Cummings "Human Heredity Principles and issues" p. 104.
  3. April Holladay (2001-05-09). "What triggers twinning?". WonderQuest. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-14. Iliwekwa mnamo 2007-03-22.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapacha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.