Juan F. Acosta
Juan F. Acosta (27 Mei 1890 - 1968) alikuwa mtunzi na mwalimu wa muziki wa Puerto Rico.
Maisha ya awali
haririAcosta, alizaliwa na kusomeshwa katika mji wa San Sebastián, ulioko upande wa magharibi wa Puerto Riko. Wazazi wake, waligundua kuwa mtoto wao alikuwa na kipaji cha muziki, katika umri mdogo walimpeleka kuchukua masomo ya muziki.
Alikuwa chini ya ufundishaji wa mwalimu Jesus Fiqueroa (1878–1971), mtunzi mahiri ambaye alimfundisha jinsi ya kucheza ala mbalimbali za muziki, miongoni mwao zikiwemo klarineti na eufoniumu . Kufikia 1900, Acosta alipokuwa na umri wa miaka 10 tu, aliweza kutayarisha muziki kwa ajili ya kuchezwa na watu katika kundi iliyoongozwa na Fiqueroa.
Mnamo 1906, alipokuwa na umri wa miaka 16, Acosta alifikiwa na mkurugenzi wa Bendi ya Manispaa ya San Sebastian, Ángel Mislan (1862-1911) ambaye alimchukua chini na kuishi naye. Mislan alimfundisha Acosta sanaa ya utunzi wa muziki. Kila mji ulikuwa na Bendi ambayo ilicheza katika uwanja wa mji. Nafasi ya mkurugenzi wa Bendi ilionekana kuwa muhimu sana na Mislan alipoondoka San Sebastian, alipendekeza Acosta awe mrithi wake. [1] [2] [3]
Utunzi wa kwanza
haririAcosta alikuwa na mpenzi wake aliyeitwa Carmela ambaye naye alikuwa na rafiki mwingine kwa jina hilohilo moja. Kabla ya kuhama kutoka San Sebastian, mwaka 1909, akiwa na umri wa miaka 19, aliandika danza yake ya kwanza iliyoitwa Las Carmelas, iliyoongozwa na wasichana. Alihamia mji wa Adjuntas ambako alipanga bendi yake ya manispaa na bendi mbalimbali za shule. Pia ndipo alipokutana na mke wake mtarajiwa, Ramonita Nieves. [1] [2]
Kipaji ama talanta ya Acosta ilifika katika sehemu nyingine za Puerto Rico na akajikuta akifanya kazi na kutembelea miji mingine kufanya kazi. Mmoja wa wanafunzi wake alikuwa kijana kwa jina la Rafael Alers, ambaye katika siku zijazo pia ameonekana angekuwa mwanamuziki mashuhuri. Alitembelea zaidi ya miji 37, ambapo aliwafundisha walimu katika muziki na kusaidia kuendeleza mfumo wa muziki wa elimu katika mashule. [1] [2]
Mnamo Julai 7, 1936, Acosta alipokuwa amepumzika chini ya mti wa msonobari kwenye uwanja wa mji wa Hatillo, kulimtia moyo kuandika moja ya nyimbo zake kuu, danza Bajo La Sombra de un Pino (Chini ya Kivuli cha Msonobari). Miongoni mwa tungo nyingi za Acosta ni Asi es la Vida (That's Life); na " Glorias del Pasado " (Utukufu wa Zamani). Acosta aliandika zaidi ya vipande 844 vya muziki, pamoja na nyimbo 127. [1] [2]
Miaka ya baadaye
haririJuan F. Acosta alikufa mwaka 1968 na kuzikwa Quebradillas . Kulingana na matakwa yake, familia yake ilipanda mti wa msonobari kando ya kaburi lake. Zaidi ya nyimbo 300 za muziki za Acosta zinalindwa katika Taasisi ya Utamaduni wa Puerto Rico. Katika miaka ya 1960, Taasisi ilirekodi nyimbo 12 bora zaidi za Acosta, zilizofasiriwa kwa piano na Elsa Rivera Salgado (1908-1998). [1] [2]
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Juan F. Acosta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |