Kipaji
Kipaji (kutoka kitenzi "ku-pa"; kwa kuwa watu wa dini huamini kipaji mtu hupewa na Mungu katika uumbaji) ni sehemu ya uwezo wa kufanya jambo fulani kwa ngazi ya juu. Kipaji kinaweza kuwa cha kimwili au cha kiakili.
Kipaji ni uwezo wa kuzaliwa nao wa kufanya kazi fulani lakini kinaweza kikandelezwa au kutoendelezwa. Kipaji hakirithishwi wala huwezi kujifunza sehemu yoyote.
Ni uwezo, ujuzi ulioendelezwa, maarifa au uhodari na mtazamo alionao mtu.
Asili ya ndani ya kipaji ni kuonyesha ujuzi na mafanikio, ambayo huwakilisha maarifa au uwezo unaopatikana kupitia kujifunza.
Kipaji huweza kuishi ndani ya mtu bila kupotea. Kadiri kinavyozidi kutumiwa ndivyo huzidi kuimarika.
Mfano wa vipaji ni: kuchora, kutambua na kuvumbua vitu kwa haraka.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |