Juliana Daniel Shonza

Mwanasiasa wa Tanzania
(Elekezwa kutoka Juliana Shonza)

Juliana Daniel Shonza (alizaliwa 23 Aprili 1987) ni mwanasiasa wa Tanzania na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi( CCM). Kwa sasa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pia ni Mbunge wa kuteuliwa kupitia nafasi ya Viti maalumu ndani ya Bunge la Tanzania.

Juliana Daniel Shonza
Naibu Waziri Mhe. Juliana Shonza
Naibu Waziri Mhe. Juliana Shonza
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Bunge la Tanzania
Jimbo la uchaguzi Viti maalumu
Tarehe ya kuzaliwa 23 Aprili 1987
Mahali pa kuzaliwa Mbeya
Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Tar. ya kuingia bunge 2015
Mbunge
Alingia ofisini Octoba 2017
Aliondoka ofisini 2020
Dini Mkatoliki
Elimu yake
Digrii anazoshika Shahada ya pili ya Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu cha Dodoma
Kazi mwanasiasa


Elimu na maisha binafsi

hariri

Juliana Shonza alizaliwa katika mkoa wa Mbeya. Mwaka 1995 alianza elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Sinde.[1] Alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Kibasila mwaka 2005 na baadaye kuhitimu kidato cha sita shule ya sekondari Dakawa mwaka 2008. Mwaka 2008 alifanya Shahada yake ya kwanza ya Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye aliendelea na masomo ya Shahada ya pili katika fani hiyo mwaka 2013 kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.

Juliana Daniel Shonza alianza kushiriki katika siasa wakati akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 2010 akiwa chuoni hapo alianzisha umoja wa wanafunzi wa Chama Chama Demokrasia na Maendeleo Chadema CHASO na baadae kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti taifa wa Baraza la Vijana la Chadema BAVICHA.

Mwaka 2013 aliamua kuhamia Chama Cha Mapinduzi ambapo baaaae akateuliwa na Mwenekiti wa CCM wa kipindi hicho Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Katibu msaidizi wa wa motisha katika makao makuu ya CCM. Wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015, Juliana Shonza aliteuliwa kuwa Mbunge wa bunge la Tanzania kupitia nafasi ya viti maalum vya wanawake bungeni.

Baadaye, Juliana Shonza mnamo mwaka 2017 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Rais John Magufuli katika mabadiliko aliyoyafanya tarehe 9 Oktoba 2017. [2] Ni Mtumishi katika baraza la mawaziri chini ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe. [3]

Marejeo

hariri
  1. [1], Tovuti ya Bunge la Tanzania
  2. [2], PRESIDENT John Magufuli yesterday announced a cabinet reshuffle, creating two new ministries and nominating five new deputy ministers
  3. "Taarifa toka Ikulu na Gerson Msigwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-11. Iliwekwa mnamo 2018-06-20.