Jungle Brothers
Jungle Brothers ni kundi la muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Hawa hutazamwa kama waazilishi wa hip hop yenye mchanganyiko wa jazz na kuwa kama kundi la kwanza la hip hop kutumia muziki wa house katika hali ya hip-hop na kumtumia mtayarishaji wa muziki huo katika kazi zao. Kundi lilianza kutumbuiza katikati mwa miaka ya 1980 na wakafanikiwa kutoa albamu yao ya kwanza, Straight Out the Jungle, mnamo mwezi wa Julai 1988.[1] Kwa mtindo wa kutengeneza biti na mashairi yenye asili ya Kiafrika, kina Jungle Brothers wakawa maarufu mno na punde wakaungana na kundi lenye athira kubwa katika hip hop la Native Tongues.[2] Wanachama wa awali unaunganishwa na Michael Small (Mike Gee), Nathaniel Hall (Afrika Baby Bam, kwa heshima ya Afrika Bambaataa) na Sammy Burwell (DJ Sammy B). Sammy B aliondoka kundini baada ya kundi kutoa Raw Deluxe in Mei 1997.[1]
Jungle Brothers | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | New York City, Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop, alternative rap, house, hip house |
Miaka ya kazi | 1987–hadi sasa |
Studio | Idlers/Warlock Records Warner Bros. Records Gee Street/V2/BMG Records Jungle Brothers XYZ Records |
Ame/Wameshirikiana na | A Tribe Called Quest De La Soul Queen Latifah Monie Love Black Sheep Chi-Ali |
Wanachama wa sasa | |
Mike Gee Sammy B Afrika Baby Bam | |
Wanachama wa zamani | |
Torture |
Diskografia
hariri- Straight out the Jungle (1988), Warlock
- Done by the Forces of Nature (1989), Warner Bros.
- J Beez Wit the Remedy (1993), Warner Bros.
- Raw Deluxe (1997), Gee Street/V2/BMG Records
- V.I.P. (2000), Gee Street/V2/BMG Records
- All That We Do (2002), Jungle Brothers
- You in My Hut Now (2003), XYZ
- This is... (Greatest hits) (2005), Nurture Records/Groove
- I Got You (2006), Pinoeer Records[1]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 Strong, Martin C. (2000). The Great Rock Discography (tol. la 5th). Edinburgh: Mojo Books. uk. 523. ISBN 1-84195-017-3.
- ↑ Jungle Brothers katika Allmusic