Monie Love
Simone Gooden (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Monie Love; amezaliwa 2 Julai 1970) ni emcee kutoka nchini Uingereza na mtangazaji wa redio wa zamani huko nchini Marekani.
Monie Love | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Simone Gooden |
Pia anajulikana kama | Monie Love |
Amezaliwa | 2 Julai 1970 |
Asili yake | London, England |
Aina ya muziki | Hip hop BritHop New jack swing |
Kazi yake | Rapa, mwimbaji wa hip hop |
Miaka ya kazi | 1989–hadi sasa |
Studio | Warner Bros. Records Cooltempo/Chrysalis/EMI Records Tuff Groove |
Ame/Wameshirikiana na | Native Tongues Dave Angel |
Alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika hip hop ya Kiingereza, na kuleta mgongano/athira kubwa na wasaili/maemcee wengine wa kike wa Kimarekani kama vile Queen Latifah, vilevile kupitia uanchama wake na baadhi ya makundi mwishoni mwa miaka ya 1980/mwanzoni mwa miaka ya 1990 - Native Tongues. Love alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza wa BritHop kuingia mkataba na kusambaziwa kazi zake dunia nzima na mastudio makubwakubwa duniani.
Miaka ya awali
haririLove alizaliwa katika eneo la Battersea la mjini London. Huyu ni mdogo wake mwnamuziki wa muziki wa techno Dave Angel, na alikuwa binti wa baba aliyekuwa akipiga muziki wa jazz kutoka mjini London.
Shughuli za muziki
haririLove alizanza kazi yake ya hip hop/BritHop akiwa kama emcee kwenye kundi la Kiingereza la Jus Bad, kundi ambalo linaunganishwa na DJ Pogo, Sparki, na MC Mell'O'. Kundi hilo lilitoa kibao cha kilichokwenda kwa jina la "Free Style/Proud" katika studio moja ya kujitegemea Tuff Groove mnamo 1988.
Love alianza kujipatia umaarufu wake wa kujulikana kibiashara nchini Marekani baada ya kuuza sura katika single ya Queen Latifah iliyojishindia Grammy Award "Ladies First," vilevile kwenye kibao cha Adeva "Ring My Bell," na kwa kina Jungle Brothers' "Doin' Our Own Dang," na kibao kikali cha kina De La Soul "Buddy." Umaarufu huo umepelekea kuingia mkataba na Warner Bros. Records, inamfanya Love kuwa miongoni mwa wasanii wachacha sana wa British hip-hop kufanya juhudi za kutoa kazi zao na mastudio makubwakubwa duniani.
Diskografia
haririAlbamu zake
haririMwaka | Jina | Nafasi ya chati | |
---|---|---|---|
U.S. | U.S. R&B | ||
1990 | Down to Earth
|
109 | 26 |
1993 | In a Word or 2
|
– | 75 |
EP/Single alizofanya akiwa kivyake
haririMaelezo ya Albamu |
---|
Slice Of Da Pie EP
|
Single Alizoshirikishwa
hariri- "Ladies First" (Queen Latifah akiwa na Monie Love)
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- [Monie Love katika Allmusic AllMusic.com Biography - Monie Love]
- Monie Love's myspace.com page
- Monie Love Discography on Discogs
- A site focusing on the early days of Hip Hop development in the UK