Kakenya Ntaiya
Kakenya Ntaiya (alizaliwa mnamo 1978[1]) ni mtoa elimu na mwanaharakati wa masuala ya kijamii kutoka nchini Kenya.
Ni mwanzilishi na raisi wa kituo cha elimu kijulikanacho kama Kakenya Center for Excellence na shule ya bweni ya msingi kwa wanawake ipatikanayo kijji cha Wamasai kiitwacho Enoosaen[2]. Darasa lake la kwanza lilichukua takribani wanafunzi 30 mwaka 2009. Kituo kina simamia muongozo kwamba wazazi hawatakiwi kuwakeketa watoto wao wala kuwalazimisha kuolewa.[3]
Maisha yake ya awali na Elimu
haririNtaiya ni mtoto wa nane kwenye familia yao. Kutokana na mila na desturi za kimaasai Ntaiya alitakiwa kuchumbiwa akifikisha takribani umri wa miaka mitano,kufanyiwa ukeketaji, na pia kuacha shule ili aolewe. Badala yake alikubaliana na baba yake ya kuwa atakubali kufanyiwa ukeketaji ila tu aruhusiwe kuendelea na masomo yake na kumaliza elimu yake ya juu.
Marejeo
hariri- ↑ "Saving Girls: Kakenya Ntaiya Is a CNN Hero". HuffPost (kwa Kiingereza). 2013-10-24. Iliwekwa mnamo 2022-02-16.
- ↑ Kakenya's Dream | Empowerment (kakenyasdream.org)
- ↑ "Kenyan girl exchanged genital mutilation for education", ABC News (kwa Australian English), 2015-02-25, iliwekwa mnamo 2022-02-16