Kalenda ya Kichina

Kalenda ya Kichina ni kalenda ya kidesturi inayoitwa pia kalenda ya Han. Inatumiwa nchini China na pia na watu wanaofuata utamaduni wa kichina penginepo duniani pamoja na Kalenda ya Gregori.

Matumizi ya kalenda ya Kichina

hariri

Mambo ya serikali na mipango ya kiuchumi hufuata kalenda ya Gregori. Lakini sikukuu za kidesturi zinafuata kalenda ya Kichina, kwa mfano mwaka mpya wa Kichina. Kalenda hii hutumiwa pia kwa kupanga tarehe za arusi, mazishi au kuhamia nyumba kwa sababu Wachina wengi huamini kuna tofauti kati ya siku za bahati nzuri na bahati mbaya.

Mpangilio wa kalenda

hariri

Kalenda wa Kichina inafuata mwendo wa mwezi pamoja na mwendo wa jua kwa hiyo inaunganisha tabia za kalenda ya mwezi na kalenda ya jua.

Kwa kawaida mwaka mmoja huwa na miezi 12 lakini kuna pia miaka yenye miezi 13 - hii inatokea mara saba katika kila kipindi cha miaka 19. Kila mwezi unaanza kwenye siku ya mwezi mwandamu.

Muda wa mwaka wa kawaida ni siku 353 - 355. Kama ni mwaka una miezi 13, muda wake ni siku 383 - 385.

Mwaka mpya hutokea kati ya Januari 21 na Februari 21.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kalenda ya Kichina kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.