Kampuni ya Hoteli za Eppley

Kampuni ya Hoteli za Eppley inapatikana katika mji wa Omaha, Nebraska. Wakati wa kununuliwa kwake na Shirika laSheraton katika mwaka wa 1956, ilikuwa ndiyo biashara ya hoteli kubwa kabisa nchini Marekani.

Hoteli ilimilikiwa na tajiri Eugene C. Eppley,kampuni yenyewe ikiwa imeanzishwa katika mwaka wa 1917. Kulikuwa na hoteli 22 katika kampuni hii zilizoenea katika majimbo sita.

Mali zilizomilikiwa

hariri

Hoteli 22 za kampuni hii zilihusu: hoteli iliyo Pittsburgh ya William Penn, hoteli iliyo Louisville,Kentucky ya Seelbach, na ho Hoteli ya 22 katika Eppley Hotel Company's kwingineko included Pittsburgh 's William Penn Hotel, ya Seelbach Hotel katika Louisville, Kentucky na Hotel Fontenelle katika Omaha, Nebraska.

Pamoja na mali nyingine kama hoteli ya West katika Sioux City,Iowa iliyoundwa katika mwaka wa 1903 na ikawa moja ya hoteli za Eppley katika miaka ya 1930. Hoteli hiyo ya West ilichomeka kabisa katika mwaka wa 1953. Hoteli ya Warrior iliyo Sioux City iliundwa chini ya jina la "Hoteli ya Fontenelle" katika mwaka wa 1930. Eppley ilinunua Warrior katika mwaka wa 1936. Kampuni ya Eppley ikauza Warrior kwa Shirika la Sheraton ya Marekani katika mwaka wa 1956. [3]

Hoteli ya Fontenelle ya Omaha ilijengwa katika mwaka wa 1914. Ikiwa pahala maridadi sana,Fontenelle, na ikahudumia wateja maarufu na waliojulikana kama rais wa Marekani,Harry S. Truman na John F. Kennedy. Baada ya kuuzwa na Eppley kwa shirika la Sheraton, hoteli hiyo,Fontenelle, hatimaye ikaanza kuharibika ,ikafungwa katika mwaka wa 1970. Mwishowe,ikabomolewa katika mwaka wa 1983.

Katika mwaka wa 1927, Eppley ilinunua michoro ya rangi ya Grant Woods ya hoteli zake zilizokuwa Council Bluffs,Cedar Rapids,Waterloo na Sioux City. Mchoro wa awali uliochorwa kwa lengo la kuwekwa kwenye chumba cha maakuli cha Hoteli ya Martin, imehifadhiwa katika Kituo cha Sanaa cha Sioux City.

Hoteli za Eppley

hariri
 
Hoteli Fontenelle, ilipatikana Omaha, Nebraska tangu 1915 hadi 1983.
 
Hoteli ya Carpenter(sasa) ambayo ilikuwa mojawapo ya hoteli za kampuni ya Eppley
 
Hoteli ya Alexandria(sasa) iliyokuwa moja ya hoteli za kampuni ya Eppley huko Los Angeles,California
Hoteli zilizokuwa katika kundi la Eppley
Jina Jiji Maelezo
Hoteli ya Norfolk Norfolk, Nebraska
Hoteli ya Lincoln Lincoln, Nebraska
Hoteli ya Capital Lincoln, Nebraska
Hoteli ya Lindell Lincoln, Nebraska
Hoteli ya Fontenelle Omaha, Nebraska Ilijengwa katika mwaka wa 1914,hii ndiyo iliyokuwa hoteli bora kabisa katika eneo la Omaha kwa zaidi ya miaka 50.Ilibomolewa katika mwaka wa 1983.
Hotel ya Rome Omaha, Nebraska
Hoteli ya Logan Omaha, Nebraska
Hoteli ya Cataract Sioux Falls, South Dakota
Hoteli ya Carpenter Sioux Falls, South Dakota
Hoteli ya Warrior Sioux City, Iowa
Hoteli ya Martin Sioux City, Iowa
Hoteli ya West Sioux City, Iowa
Hoteli ya Tallcorn Marshalltown, Iowa
Hoteli ya Chieftain Council Bluffs, Iowa
Hoteli ya Montrose Cedar Rapids, Iowa
Hoteli ya Magnas Cedar Rapids, Iowa
Hoteli ya Seelbach Louisville, Kentucky
Hoteli ya Fort Pitt Pittsburgh, Pennsylvania
Hoteli ya William Penn Pittsburgh, Pennsylvania
Hoteli ya Alexandria Los Angeles, California
Hoteli ya Elms Hotel Excelsior Springs, Missouri

Muungano

hariri

Eugene Eppley aliiuza kampuni ya Eppley kwa Hoteli za Sheraton katika mwaka wa 1956 kwa bei ya $ milioni 30. Huo ndio uliokuwa bei ghali ya pili katika uuzaji wa hoteli katika historia ya Marekani, wakati huo.

Angalia pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Closing the Gap" Ilihifadhiwa 24 Mei 2009 kwenye Wayback Machine., Time magazine. 4 Juni 1956.
  2. Take a step back in time: Nebraska Street walking tour Ilihifadhiwa 8 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.. Sioux City Museum.
  3. "Closing the Gap" Ilihifadhiwa 24 Mei 2009 kwenye Wayback Machine., Time magazine. 4 Juni 1956..

Viungo vya nje

hariri