Kampuni ya Rockport

Kampuni ya Rockport ni kampuni ya kutengeneza viatu iliyo na makao yake katika eneo la Massachusetts. Ilianzishwa huko Marlborough, Massachusetts katika mwaka wa 1971 na Saul na Bruce Katz, kampuni hii inaendelea kutengeneza viatu na huendesha maduka nchini Marekani na nchi 66 duniani kote. Kampuni hii ilinunuliwa na kampuni ya Reebok katika mwaka wa 1984. Hivi sasa,kampuni zote mbili zinamilikiwa na kampuni kubwa ya Ujerumani ya Adidas. Kampuni ya Rockport ,hivi sasa, ina makao yake mjini Canton, Massachusetts, katika makao makuu ya Reebok.

Duka la Rockport lililopo Newport, Rhode Island
Kampuni ya Rockport
Jina la kampuni Kampuni ya Rockport
Ilianzishwa 1971, Marlborough, Massachusetts
Mwanzilishi Saul Katz
Bruce Katz
Mmiliki Kampuni ya Reebok
Makao Makuu ya kampuni Canton, Massachusetts
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Viatu vya aina mbalimbali
Viatu vya Wanaume
Viatu vya Wanawake
Viatu vya Watoto
Nchi Marekani
Tovuti http://www.rockport.com/

Historia

hariri

Rockport ilianzishwa katika mwaka wa 1971 na muungano wa baba na mwana (Saul na Bruce Katz) katika eneo la Marlborough, Massachusetts. Saul na Bruce waliamua kwamba kuwa kile kilichokosekana katika sekta ya viwanda vya viatu ni viatu vilivyohusisha kuwa na uzito mdogo,faraja na mitindo mzuri. Hizi ndizo sifa ambazo zingehusishwa na viatu vya Rockport katika mwongo uliofuata.

Katika mwaka wa 1984, kampuni hii ilinunuliwa na kampuni ya viatu ya Reebok. Huu ndio uliokuwa hatua dhahiri ya Reebok kuingia katika utengenezaji wa viatu visivyokuwa vya michezo. Rockport ilifaidika kwa hela zilizotokana na ununuzi huo na pia kutoka teknolojia ya kampuni ya Reebok iliyotumika katika kutengeneza viatu vya ofisi na vya matembezi. Hii ingesababisha matumizi, ya baadaye, ya soli za ndani za faraja za DMX katika viatu vingi vya Rockport.

Rockport hutengeneza viatu mbalimbali kama viatu vya oxford,viatu vya mchezo wa golfu, viatu vya boat shoes, viatu vya matembezi na aina vingine mbalimbali. Hivi vinapatikana katika mitindo ya wanaume, wanawake na ,mara nyingine, ya watoto. Viatu maarufu kabisa kati ya hivi vyote ni vile vya ProWalker, viatu vilivyokuwa na soli ngumu sana.Aina hii ilikuwa mojawapo ya viatu vya kwanza vya Rockport.

Teknolojia zao

hariri

Rockport hutangaza kuwa wao ndio viongozi kiteknolojia katika utengenezaji wa viatu. Bidhaa zao za kiteknolojia ni DMX, WalkDry, XCS na soli ya Vibram.

Teknolojia ya DMX inahusisha kutia hewa ndani ya soli ya nje ya kiatu au ndani ya soli ya ndani. Hii inazuia madhara madogo kwa mguu unapochukua hatua.

WalkDry

hariri

Viatu vilivyotumia teknolojia ya WalkDry huwa na ngozi isiyopitisha maji na huruhusu kupita kwa hewa; ni kama teknolojia ya Gore Tex.

Soli ya Vibram

hariri

Soli ya Vibram zimebainika katika masoko yote ya viatu kuwa soli zilizodumu kabisa. Lengo lake huwa kuwa dhabiti lakini bado kuwa na faraja.

XCS inamaanisha Extreme Conditions System katika lugha ya Kiingereza. Hii ni kumaanisha mfumo unaoweza kustahimili hali ngumu.Teknolojia ya XCS hutumika katika viatu vyote vya nje vya Rockport, na hupambana na shida za kukwaruzwa na kuingiwa na maji.

Viungo vya nje

hariri