Karani tamba
Karani tamba | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Karani tamba
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Karani tamba (Sagittarius serpentarius) ni ndege mkubwa wa ardhini ambaye huwinda wanyama wengine. Yeye hupatikana katika maeneo mengi Barani Afrika, mara nyingi katika maeneo tambarare na katika maeneo ya nyika ya Afrika.
Ingawa anaainishwa katika oda ya Accipitriformes, ambayo ni ya ndege wengi wawindaji wanaoonekana mchana kama vile mwewe, shakivale, tai na kipondya, karani tamba amepewa familia yake ya kipekee iitwayo Sagittariidae.
Ndege huyu huonekana katika nembo ya nchi za Sudan na Afrika Kusini.
Sifa
haririKarani tamba anafahamika wazi kutokana na mwili wake unaofanana wa tai, na miguu yake inayofanana ya korongo, inayomfanya aonekana mrefu zaidi hata kufikia urefu wa mita 1.3 (futi 4). Ndege huyu mwenye urefu wa sentimita 140 (futi 4.5) ana kichwa kinachofanana cha tai na mdomo uliojipinda kwenda chini, lakini ana mabawa ya mviringo.
Uzani wake wa wastani ni kilo 3.3 (paundi 7.3) na upana wa mabawa ni mita 2 (futi 6.6).
Kwa umbali au anapopaa angani, yeye hufanana korongo bali si ndege wa kuwinda. Mkia una manyoya mawili marefu yanayoonekana kuwa marefu kuliko miguu yake anapopaa, na pia ana mkusanyiko wa manyoya yanayotengeneza umbo kama la nundu. Manyoya ya kupaa ya karani tamba na mapaja yake ni meusi, huku manyoya mengine yakiwa rangi ya kijivu na mengine yakiwa meupe.
Marejeo
hariri- Tanzaniabirds.net: Secretary bird
Makala hii kuhusu ndege fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Karani tamba kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |