Kivunjajungu

(Elekezwa kutoka Katamasikio)
Kivunjajungu
Kivunjajungu kijani wa Ulaya (Mantis religiosa)
Kivunjajungu kijani wa Ulaya (Mantis religiosa)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda ya juu: Dictyoptera
Oda: Mantodea
Burmeister, 1838
Ngazi za chini

Familia 16:

Vivunjajungu, vunjajungu au katamasikio ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Mantodea (mantis = nabii, eidos = umbo) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki na kusini (au kaskazini) kwa kanda za wastani. Kiwiliwili chao ni kirefu na chembamba. Miguu ya mbele imetoholewa kwa kukamata arithropodi wengine na hata vertebrata wadogo. Kwa kawaida koksa (coxa) za miguu ya wadudu ni fupi, lakini zile za miguu ya mbele ya vivunjajungu zimerefuka. Femuri na tibia zina miiba na meno inayowezesha mdudu kushika vizuri mawindo yake. Kama takriban wadudu wote vivunjajungu wana toraksi yenye sehemu tatu, lakini ile ya mbele, protoraksi, ni ndefu kuliko mbili nyingine pamoja na imeungwa vinamo na mesotoraksi. Hii inawezesha mdudu asogeze kichwa na miguu ya mbele pande zote wakati kiwiliwili kinatulia. Hata shingo ni kinamo na spishi kadhaa zinaweza kuzungusha kichwa kwa nyuzi 180.

Mabadiliko ya mguu wa mbele: koksa ni ndefu sana na inafanana na femuri. Femuri binafsi ni kiungo cha kwanza cha sehemu ya kukamata ya mguu.
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kivunjajungu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.