Katrin Meissner

Mwandishi wa Ujerumani na Australia na mwanasayansi wa hali ya hewa, mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa katika Chuo Kikuu cha New South Wales

Katrin Juliane Meissner ni mwanafizikia anayesomea utafiti wa hali ya kimwili na michakato ya kimwili ndani ya bahari, hasa mienendo na sifa za kimwili za maji ya bahari pamoja na utafiti wa kisayansi wa hali ya hewa ya dunia.Ambayo inayojulikana kwa mifano ya hali ya hewa inayotathmini athari za mabadiliko ya hali ya hewa ya ghafla kwenye mizunguko ya ardhini na baharini ya biogeochemical.

Katrin Meissner

Elimu hariri

Meissner alikulia Berlin, Ujerumani, ambako alihudhuria shule ya Gymnasium ya Französisches Berlin.Meissner alimaliza digrii ya uhandisi katika Ecole Centrale de Lille mnamo 1995.Baadae Meissner alihamia chuo kikuu cha Pierre et Marie Curie, Paris VI, Ufaransa ambapo alianza uchunguzi wa kutabirika kwa monsuni za Afrika ya mangaribi kulingana na mitiririko ya hali ya hewa itokayo pwani ya Senegal.Meissner alipokea Ph.D. katika Taasisi ya Alfred Wegener ya Utafiti wa Polar na Marine katika Universität Bremen, Ujerumani mnamo 1999. Alitengeneza kielelezo cha angahewa na kielelezo cha barafu ya baharini na akaunganisha zote mbili kwa modeli iliyopo ya bahari ili kujifunza kubadilika kwa muda mrefu kwa mzunguko wa thermohaline. Kwa kazi hii alipokea Tuzo la Annette Barthelt kwa utafiti bora katika uwanja wa sayansi ya baharini mnamo 2000. Meissner alikamilisha postdoc katika Chuo Kikuu cha Victoria, Kanada, 2000-2002 na baadaye alikuwa Profesa Msaidizi huko katika Shule ya Sayansi ya Dunia na Bahari kuanzia 2002 hadi 2009. Mnamo 2009, alihamia Chuo Kikuu cha New South Wales, Sydney, Australia.Kuhamishwa kwake kutoka kwa nafasi ya umiliki huko Chuo Kikuu Cha Victoria kulitokana na masuala ya muda mrefu ya kupunguza ufadhili wa sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa kote Kanada. Mnamo 2010, alitunukiwa Tuzo ya Ushirika wa Baadaye wa Baraza la Utafiti la Australia. Mnamo 2020 aliitwa Mshirika wa Jumuiya ya Kifalme ya New South Wales (FRSN). Kufikia 2021, alikuwa ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Mabadiliko ya Tabianchi na ana wadhifa wa Profesa Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Victoria, Kanada na wadhifa wa uungwana katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Oregon. Yeye ni mwanachama wa Kamati ya Wataalamu ya Mkakati wa Ubora wa Ujerumani. Meissner yuko katika kamati inayosimamia mradi wa PAGES (Past Global Changes) ambao huratibu na kukuza utafiti wa mabadiliko ya tabianchi. Mnamo 2015, alikuwa mmoja wa wanasayansi walioangaziwa katika mradi wa Joe Duggan kuhusu hisia za wanasayansi ambao kazi yao inaangazia mabadiliko ya hali ya hewa.Mradi huu ulifuatiliwa mwaka wa 2020.Meissner pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa katika kipindi cha Lateline cha ABC mwaka wa 2017 na katika makala ya maoni katika Sydney Morning Herald. Yeye ni mhakiki hai wa "Maoni ya Hali ya Hewa" kwa Media Watch ya ABC. Mnamo Juni 2018, alikuwa mwandishi mwenza wa karatasi katika Sayansi ya Jiolojia ambayo iliweka kwamba makadirio ya hali ya hewa ya sasa ya msingi yanaweza kudharau sana kiwango cha ongezeko la joto.

Utafiti hariri

Eneo kuu la utafiti wa Meissner's na ushiriki wa kisayansi ulijikita katika mabadiliko ya hali ya hewa. Akiwa katika chuo kikuu cha Victoria, alikumbana na mfano wa mmea pamoja na mpango wa uso ardhi na anga hewa la bahari barafu-na mfano wa hali ya hewa ya barafu na alianzisha vifuatiliaji kadhaa vya isotopiki katika mfano wa hali ya hewa ili kuwezesha kulinganisha na paleoproxies katika kumbukumbu za hali ya hewa. Katika utafiti wake wa juu ya matukio ya ghafla ya mabadiliko ya hali ya hewa,Meissner's aliunda na kuunganisha vipengele kadhaa kwa Miundo ya Hali ya Hewa ya Mfumo wa Dunia iliyopo ambayo husaidia kuwezesha ulinganisho na kumbukumbu za hali ya hewa za zamani na kujumuisha michakato changamano ya ardhi katika mifano hiyo. Pia Meissner's alichanganya mifano ya hali ya hewa na rekodi za hali ya hewa ya palaeoclimate ili kuongeza uelewa wa mifumo ya msingi ya kutofautiana kwa hali ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa,Hususani katika muktadha wa mizunguko ya kibaiolojia na kikemikali baharini na ardhini, usambazaji wa bahari,na mabadiliko ya mazingira ya kemikali ya miamba ya matumbawe.Kazi yake(Meissner's) na timu yake iliendeleza masomo ya mfano juu ya mabadiliko ya haraka ya hali ya hewa nchini Australia[1] [2] [3] [4] [5] [6] [7] [8]

Marejeo hariri

  1. "SSC membership history". pastglobalchanges.org (kwa en-gb). Iliwekwa mnamo 2021-05-08. 
  2. Perkins-Kirkpatrick, Sarah. "How should we feel about climate change? | Inside Story", Inside Story, 2015-09-23. (en-US) 
  3. "'I'm profoundly sad, I feel guilty': scientists reveal their personal fears about the climate crisis". the Guardian (kwa Kiingereza). 2020-03-07. Iliwekwa mnamo 2021-03-12. 
  4. Brewster, Kerry (2017-06-27), Climate scientists reveal their fears for the future (kwa en-AU), Australian Broadcasting Corporation, iliwekwa mnamo 2021-03-12 
  5. "The Sydney Morning Herald", The reef report is in and ocean scientists are fearful, August 30, 2019. 
  6. "Ep 42 - the Australian defends Plimer". Australian Broadcasting Corporation. 2 December 2019.  Check date values in: |date= (help)
  7. Fischer, Hubertus; Meissner, Katrin J.; Zhou, Liping (25 June 2018). "Palaeoclimate constraints on the impact of 2 °C anthropogenic warming and beyond". Nature Geoscience 11 (7): 474–485. Bibcode:2018NatGe..11..474F. doi:10.1038/s41561-018-0146-0.  Unknown parameter |s2cid= ignored (help); Check date values in: |date= (help)
  8. Cimons X., Marlene (2018-07-19). "The Climate Has Always Changed. Why Is This Time so Much Worse?". Nexus Media News (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2021-03-12. 
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Katrin Meissner kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.