Bremen ni mji wenye bandari muhimu katika Ujerumani ya Kaskazini. Iko kando ya mto Weser takriban km 50 kabla haujaingia katika Bahari ya Kaskazini. Mto Weser unapanuka baada ya kupita mji kuwa na mdomo mpana sana kabla ya kuishia baharini hivyo meli zinaweza kufika hadi mjini.

Die Bremer Stadtmusikanten bei Nacht.


Bremen
Bremen is located in Ujerumani
Bremen
Bremen

Mahali pa katika Ujerumani

Majiranukta: 53°04′33″N 08°48′27″E / 53.07583°N 8.80750°E / 53.07583; 8.80750
Nchi Ujerumani
Jimbo Bremen
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 547,685
Tovuti:  http://www.bremen.de/
Nembo ya Bremen

Mji una wakazi 546,000. Pamoja na eneo la jirani kuna watu milioni 2.37 katika mazingira ya Bremen.

Bremen ni dola-mji ikiwa moja ya majimbo 17 ya kujitawala ya Ujerumani. Jina rasmi ni „Mji huru wa Hanse wa Bremen“ (Freie Hansestadt Bremen). Hanse ilikuwa shirikisho la kimataifa la miji ya biashara iliyojitawala katika karne za kati. Kwa muda mrefu wa historia yake Bremen ilikuwa kama nchi ndogo ya kujitegemea hadi kujiunga na Dola la Ujerumani 1871. Jimbo la Bremen lina miji miwili ya Bremen yenyewe na Bremerhaven.

Wafanyabiashara wa Bremen waliwahi kuwa na biashara na nchi za nje kwa jahazi na meli zao tangu karne nyingi. Hata mawasiliano kati ya Afrika na Ujerumani yalipitia hasa Bremen na mji jirani wa Hamburg.

Picha za Bremen hariri

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bremen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.