Katuna ni mji katika Wilaya ya Kabale nchini Uganga mpakani mwa nchi ya Rwanda. Mji huu vilevile unajulikana kwa jina la Gatuna katika lugha ya Kinyarwanda[1].

Mahali hariri

Katuna inapatikana mpakani mwa Uganda na nchi ya Rwanda kusini mwa Uganda. Mji huu unapatikana ndani ya mkoa mdogo wa Kamuganguzi kaunti ya Ndorwa. Ni karibia kilometa 28 urefu wa barabara kusini Mwa Kabale, Jiji kubwa ndani ya mkoa.

Majuisho hariri

Katuna ni moja kati ya lango kubwa la kuingilia nchini Rwanda na imekua nisehemu muhimu sana ya kuingiza na kutoa bidhaa ndani na nje kati ya nchi ya Uganda na Rwanda. Bidhaa nyingi zinazoingia nchini Rwanda kutoka bandari ya Mombasa zimekuwa zikipitia boda (mpaka)ya Katuna. Kutokana na shughuri nyingi za kiuchumi na za kitalii kufanyika hapo Mji wa Katuna unakua kwa kasi sana. Mpaka wa katuna umefunguliwa masaa 24 kwa siku.

Marejeo hariri