Keir Starmer
Sir Keir Rodney Starmer (amezaliwa 2 Septemba 1962) ni mwanasiasa na wakili wa Uingereza ambaye amehudumu kama Waziri Mkuu wa Uingereza tangu 5 Julai 2024, na amekuwa kiongozi wa 19 wa Chama cha Labour tangu mwaka 2020.[1] Pia aliwahi kuwa Kiongozi wa Upinzani kutoka 2020 hadi 2024. Tangu mwaka 2015, amekuwa Mbunge wa Holborn na St Pancras, jimbo la ndani ya London. Starmer amechaguliwa tena kama Mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa 2017 na wa 2019.
Kiongozi wa Labour
haririMnamo Januari 2020, Starmer alitangaza kugombea nafasi ya Kiongozi wa Chama cha Labour katika uchaguzi wa 2020.[2] Mnamo 4 Aprili 2020, Starmer alichaguliwa kuwa kiongozi wa Chama cha Labour, na kwa kuwa Labour ilikuwa na idadi ya pili ya viti katika Bunge la Commons, alifanywa kuwa Kiongozi wa Upinzani.[3] Alishinda uongozi wa Chama cha Labour katika raundi ya kwanza ya upigaji kura kwa kutumia mbinu ya kura inayoweza kuhamishwa. Starmer alipata kura 275,780 (56.2%). Alipata asilimia 53.13% ya kura za wanachama wa vyama washirika, asilimia 56.07% ya kura za wanachama wa Chama cha Labour, na asilimia 78.64% ya kura za wafuasi waliosajiliwa.[4]
Maisha binafsi
haririStarmer ni haamini uwepo wa Mungu,[5] lakini amesema kuwa anaamini katika imani na nguvu yake ya kuwaleta watu pamoja. Mke wake, Victoria Alexander, ni Myahudi, na watoto wao wawili wanalelewa katika imani hiyo.[6]
Marejeo
hariri- ↑ "Starmer Is U.K.'s New Prime Minister". New York Times. 5 Julai 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Labour leadership: Sir Keir Starmer enters race", BBC News, 4 January 2020. (en-GB)
- ↑ "Keir Starmer Elected as new Labour leader", BBC News, 4 April 2020.
- ↑ "Leadership and Deputy Leadership election 2020 - Results". The Labour Party. 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Machi 2023. Iliwekwa mnamo 3 Oktoba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Williams, Rhiannon (11 Aprili 2021). "Keir Starmer: I may not believe in god, but I do believe in faith". inews.co.uk (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 23 Januari 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Harpin, Lee (16 Novemba 2020). Simons, Jake Wallis (mhr.). "Starmer: Our kids are being brought up to know their Jewish backgrounds". Kigezo:Ill. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Septemba 2022. Iliwekwa mnamo 3 Oktoba 2023.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
hariri- Keir Starmer on Twitter
- Official website
- CPS Archived 14 Desemba 2017 at the Wayback Machine