Keki
Keki ni chakula kinachotengenezwa kwa kuoka unga wa nafaka, maji au zaidi maziwa, sukari, soda ya kuokea pamoja na shahamu (k.m. siagi), na nyongeza nyingine kama vile mayai.
Jina latokana na neno la Kiingereza "cake" .
Keki zilianza kama mkate wa pekee ulioongezwa sukari au asali, baadaye pia shahamu au mafuta.[1]
Ilhali mwanzoni keki na mkate hazikutofautishwa sana baadaye mbinu za kuoka keki tamu ziliongezeka sana. Tangu karne ya 18 mafundi wa Ualya waliacha kutumia hamira kama mbinu wa kupata keki laini badala yake walitumia yai lililopigwa hadi kuwa pofu; katika karne ya 19 elimu ya kemia iliunda matumizi ya soda ya kuokea ambayo ni kabonati natiri (magadi) inayotoa gesi wakati wa kuoka na hivyo kuunda nafasi ndani ya kinyunga.[2]
Siku hizi kuna aina maelfu za keki.
-
Keki iliyookwa katika mviringo wa mabati
-
Keki sahili yenye mazabibu makavu
-
Keki yenye kanda za jemu ikifunikwa nje kwa ganda la siyagi tamu
Tanbihi
hariri- ↑ [The Diner's Dictionary: Word Origins of Food and Drink Cover John Ayto OUP Oxford, 18.10.2012makala "cake" katika ohn Ayto: The Diner's Dictionary, John Ayto: The Diner's Dictionary: Word Origins of Food and Drink, OUP Oxford 2012, ISBN 10: 0199640246, ISBN 13: 9780199640249, kupitia google books, iliangaliwa Julai 2017
- ↑ History of Cakes, tovuti ya Whats cooking America, ilitazamiwa Julai 2017