Kinyunga (chakula)
Kinyunga au kinyunya ni mchanganyiko wa unga wa nafaka na kiowevu hasa maji unaotarajiwa kuokwa kwenye joto.
Kuna njia mbalimbali za kukoroga kinyunga ambacho ni chanzo cha mkate, chapati, keki au maandazi. Hata spaghetti zinaanza kama aina ya kinyunga lakini zinakaushwa kwanza na kupikwa baadaye.
Kwa matumizi ya mkate wa kuoka kinyunga kinahitaji kukaa na kuchachuka. Hii inatokea kwa kuongeza dawa la chachu au kukiacha kinyunga kwa siku moja hivi na kusubiri chachu asilia ambayo ni seli za hamira hewani.
Mikate bapa mara nyingi haihitaji chachu kama kinyunga kinatumiwa kwa umbo bapa na nyembamba sana kwa vile chapati au tortilla zinazoiva juu ya bati joto tu au kwenye sufuria.
Keki ina kinyunga kizito pamoja na unga, sukari, mafuta, matunda, viungo na maziwa badala ya maji. Upande wa keki kuna pia kinyunga ya majimaji ya kufanana na uji kinachohitajika kwa keki maalumu.