Kemia kaboni

(Elekezwa kutoka Kemia mahuluku)

Kemia kaboni (pia: Kemia ya kikaboni, Kemia ogania, Kemia mahuluku; kwa Kiingereza organic chemistry) ni tawi la sayansi ya Kemia linalochunguza kampaundi za kikemia zinazojengwa na kaboni[1].

Inaitwa pia kemia ogania kwa sababu miili ya viumbehai wote inafanywa kwa maji na kampaundi ogania (= kampaundi kikaboni).

Moja kati ya tabia za kaboni ni uwezo wake wa kujiunga na elementi nyingi, hivyo kuunda molekuli kubwa. Kwa sasa kuna takriban milioni 40 za miungano ya kikemia.

Mbali na kuelewa michakato ya uhai katika miili ya viumbehai, kemia ya kikaboni imekuwa muhimu pia kwa uchumi, maana vifaa na dutu zinazidi kutengenezwa kwa kutumia kemia hii, kwa mfano madawa, uzalishaji wa nishati (biofueli) na katika fani zote za bioteknolojia.

Marejeo

hariri
  1. isipokuwa kampaundi kadhaa ambazo ni siogania (yaani hazina asili katika viumbehai) na elementi ya kaboni yenyewe

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kemia kaboni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.