Kereng'ende (ndege)

Kereng'ende
Kereng'ende koo-njano (Pternistis leucoscepus)
Kereng'ende koo-njano (Pternistis leucoscepus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Galliformes (Ndege kama kuku)
Familia: Phasianidae (Ndege walio na mnasaba na kwale)
Nusufamilia: Perdicinae (Ndege wanaofanana na sikipi)
Jenasi: Pternistis
Wagler, 1832
Ngazi za chini

Spishi 25:

Kereng'ende ni ndege wa jenasi Pternistis katika familia Phasianidae. Huitwa kwale pia pamoja na spishi nyingine za nusufamilia Perdicinae. Kwa sababu jenasi hiyo inatambuliwa kuwa na nasaba mbali kidogo na jenasi zile nyingine, sasa jina kereng'ende linapendelewa.

Rangi yao ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Ngozi ya koo na pande zote za macho ni kichele na ina rangi ya manjano, ya machungwa au nyekundu. Huonekana zaidi kuliko spishi nyingine za kwale. Chakula chao ni mbegu, wadudu na nyungunyungu. Hutaga mayai matatu hadi nane ardhini pengine juu ya manyasi makavu.

Spishi zote zinatokea Afrika.

Spishi

hariri