Kerio ni mto wa kaunti ya Turkana (zamani katika Bonde la Ufa) nchini Kenya.

Bonde la Kerio.

Chanzo chake kiko karibu na ikweta kwenye mitelemko ya ngome ya Elgeyo (Keiyo) kwenye kimo cha karibu mita 2,000.

Mto hufuata mwendo wake katika bonde la Kerio ambalo ni sehemu ya Bonde la Ufa kubwa. Mto huelekea kaskazini kati ya milima ya Elgeyo na milima ya Tugen ukipitia Marakwet na Pokot mashariki hadi kuishia katika Ziwa Turkana.

Kerio ni kati ya mito mirefu ya Kenya.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri