Kaunti ya Turkana
Kaunti ya Turkana ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Kaunti ya Turkana | |
---|---|
Kaunti | |
Mto Turkwel ukiwa umekauka wakati wa ukame | |
Turkana County in Kenya.svg Kaunti ya Turkana katika Kenya | |
Coordinates: 3°09′N 35°21′E / 3.150°N 35.350°E | |
Nchi | Kenya |
Namba | 23 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Bonde la Ufa |
Makao Makuu | Lodwar |
Miji mingine | Lokichogio, Kakuma, Lokichar |
Gavana | Jeremiah Napotikan |
Naibu wa Gavana | Peter Lotethiro Emuria |
Seneta | James Lomenen |
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Joyce Akai Emanikor |
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Turkana |
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 30 |
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 6 |
Eneo | km2 68 232.9 (sq mi 26 344.9) |
Idadi ya watu | 926,976 |
Wiani wa idadi ya watu | 14 |
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti | turkana.go.ke |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 926,976 katika eneo la km2 68,232.9 msongamano ukiwa hivyo wa watu 14 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Lodwar.
Jiografia
haririKaunti ya Turkana ndio kaunti kubwa zaidi ikiwa na km2 71 597.8 (sq mi 27 644.1). Imepakana na Uhabeshi, Sudani Kusini (kaskazini), Uganda (magharibi), Pokot Magharibi, Baringo, Samburu (kusini) na Marsabit (mashariki).
Turkana ina safu za milima: Milima Loima, Milima Lorengippi, Milima Mogila, Milima Songot, Milima Kalapata, Milima Loriu, Milima Kailong’kol na Milima Silale. Safu hizo ni vyanzo vya maji. Vilima vya Tepes, Vilima vya Lokwanamoru, Vilima vya Lorionotom, Vilima vya Pelekech na Vilima vya Loima pia hupatikana katika Turkana[2].
Tambarare za kaunti hupatikana katika sehemu kavu za kaunti.
Mto Tarach, Mto Kerio, Mto Kalapata, Mto Malimalite na Mto Turkwel ndio mito mikuu katika kaunti. Mito hii hupungua kiwango cha maji msimu wa kiangazi, na kukauka wakati wa ukame[3]. Ziwa Turkana liko mashariki mwa kaunti. Limegawanywa kati ya Turkana, Marsabit na Uhabeshi. Katika maeneo karibu na ziwa, kuna chemchemi zilizopo. Chemchemi za Eliye ndio chemchemi maarufu na kivutio cha watalii[2].
Turkana ina tabianchi kavu na nusu kavu. Kaunti hupata misimu miwili ya mvua: Aprili hadi Julai na Oktoba hadi Novemba[2].
Utawala
haririKaunti ya Turkana imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[4]:
- Kibish 36,769
- Loima 107,795
- Turkana Central 185,305
- Turkana East 138,526
- Turkana North 65,218
- Turkana South 153,736
- Turkana West 239,627
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 "SECOND ANNUAL DEVELOPMENT PLAN" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (pdf) mnamo 2018-01-27. Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
- ↑ Cheboit, Emanuel. "Crisis in Turkana as only River dries up - Citizentv.co.ke". Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
- ↑ http://countytrak.infotrakresearch.com/Turkana-county/
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Turkana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |