Kevin Peter Hall (9 Mei 1955 – 10 Aprili 1991) alikuwa mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Alifahamika sana kwa kucheza kwake katika filamu kama vile Misfits of Science, Prophecy, Without Warning, na Harry and the Hendersons. Alitambulika mno kwa kucheza uhusika wa filamu ya Predator na Predator 2.

Kevin Peter Hall
Amezaliwa (1955-05-09)Mei 9, 1955
Pittsburgh, Pennsylvania, Marekani
Amekufa Aprili 10, 1991 (umri 35)
Hollywood, Los Angeles, California, Marekani
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1979–1991
Ndoa Alaina Reed Hall (1988-1991)

Maisha ya awali

hariri

Hall alizaliwa mjini Pittsburgh, Pennsylvania.[1] Baba'ke, Marcus Alvarez, alikuwa na urefu wa futi 6' 6" na mama'ke, Sylvia Hall, alikuwa na urefu wa futi 6' 2". Kwa urefu wa 7' 2",[2] yeye alikuwa mrefu kupita wote katika familia ya wanandugu sita wa kiume, ambao wote wana zaidi ya 6' 5". Wakati wa masomo yake ya elimu ya juu katika shule ya Penn Hills High School, alifanya vyema sana katika mpira wa kikapu na kupata ufadhili wa kwenda kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha George Washington huko mjini Washington, D.C.. Akiwa chuo, Hall aliendelea kucheza mpira wa kikapu na kujikita zaidi katika Sanaa za Tamthilia.[3] Baada ya kumaliza, Hall akahamia nchini Venezuela kucheza mpira wa kikapu.

Hall amefanya igizo lake kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1979 kwenye filamo moja hivi ya kutisha ya Prophecy. Kwa kufuatia kimo chake kirefu, mara nyingi sana alicheza uhusika wa jitu la kutisha. Ameonekana kama "kiumbe cha ajabu" kwenye filamu ya kutisha ya mwaka wa 1980, Without Warning, na vilevile kacheza kama "Gorvil" kwenye filamu ya kutisha ya televisheni mnamo 1982, Mazes and Monsters. Mnamo mwaka wa 1985, amepata kucheza kama mshiriki mwenzi kwenye mfululizo mfupi wa Misfits of Science. Mwaka uliofuatia, Hall bado tena kacheza kama jitu la kutisha kwenye picha moja hivi ya kusisimua ya Monster in the Closet, ikifuatiwa na uhusika wa "Harry" kwenye Harry and the Hendersons.

Mnamo mwaka wa 1986, Hall alipata kucheza kama Predator kwenye filamu ya Predator, ambayo imechezwa na nyota Arnold Schwarzenegger. Wakati wa hatua za utengenezaji wake, Predator ilibidi ichezwe na Jean-Claude Van Damme, ambaye alicheza katika vijisehemu kadhaa vya kwanza vya Predator, lakini havikupewa kete. Watayarishaji wakaamua kuchukua mshiriki mwingine ambaye ni Hall hivyo basi Predator ameweza kuwashinda wahusika wa kawaida wa filamu. Hall akaenda tena kwenye mfululizo wa pili wa filamu ya Predator 2 mnamo mwaka wa 1990.

Kwa kufuatia uhusika wake wa kwenye Predator, Hall amepata kuonekana tena kwenye Big Top Pee-wee (1988), na alipata kuuza sura kwenye Star Trek: The Next Generation. Kuanzia 1989 hadi 1990, alikuwa na uhusika wa kujirudia kwenye ucheshi wa NBC almaarufu kama 227. Mnamo mwaka wa 1990, Hall akarudia tena uhusika wake kama Harry kwenye mfululizo wa televisheni ambao unatokana na filamu. Alikuja kufa wa msimu wa kwanza wa mfululizo.

Maisha binafsi na kifo

hariri

Hall amekutana na mwigizaji Alaina Reed wakati wanafanya matayarisho ya kipindi cha televisheni cha 227. Wawili hao waliona kwenye kipindi, halafu baadaye kwenye maisha ya kweli.[4]

Wakati anafanyia kazi katika mfululizo wa Harry and the Hendersons, Hall alitangaza kwamba alipatwa na UKIMWI baada ya kupata damu iliyoambukizwa wakati kuongezewa.[5] Mnamo tar. 10 Aprili 1991, Hall alikufa kwa kichomi.[6] Alikufa akiwa na umri wa miaka ipatayo 35.

Filmografia

hariri
Filamu
Mwaka Filamu Uhusika Maelezo
1979 Prophecy Mutant bear Uncredited
1980 Without Warning The Alien Credited as Kevin Hall
1983 One Dark Night Eddie
1984 The Wild Life Bouncer Credited as Kevin Hall
1986 Monster in the Closet Monster
1987 Harry and the Hendersons Harry
Predator The Predator/Helicopter pilot
1988 Big Top Pee-wee Big John
1990 Predator 2 The Predator
1991 Highway to Hell Charon
Televisheni
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
1982 Mazes and Monsters Gorvil Television movie
1984 E/R Donald Haines kipengele kimoja
1985 Night Court Wendell Martin kipengele kimoja
The Dukes of Hazzard Floyd Malone kipengele kimoja
1985-1986 Misfits of Science Dr. Elvin "El" Lincoln 16 episodes
1989 Rodney Dangerfield: Opening Night at Rodney's Place Richard Small Television special
Shannon's Deal Harry Filamu ya televisheni
Star Trek: The Next Generation Leyor kipengele kimoja
1989-1990 227 Warren Merriwether 1kipengele kimojas
1990-1991 Harry and the Hendersons Harry Vipengele vinne

Marejeo

hariri
  1. Kevin Peter Hall Biography (c. 1955-1991)
  2. Halliwell, Leslie (2003). Halliwell's Who's Who In the Movies (tol. la 15). HarperCollins. uk. 209. ISBN 0-0605-3423-0. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  3. Donnelley, Paul (2005-11-01). Fade To Black: A Book Of Movie Obituaries (tol. la 3). Omnibus Press. ku. 436. ISBN 1-844-49430-6.
  4. "Actor Kevin Peter Hall Dies In L.A. At Age 35". Jet. 80 (2). Johnson Publishing Company: 62. 2009-04-29. ISSN 0021-5996.
  5. Snauffer, Douglas (2008). The Show Must Go on: How the Deaths of Lead Actors Have Affected Television. McFarland. uk. 201. ISBN 0-786-43295-0. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  6. "Kevin Peter Hall, Actor, 35", New York Times, 1991-04-19. Retrieved on 2008-02-14. 

Viungo vya Nje

hariri