Kibalantak (pia Kikosian) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabalantak kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibalantak imehesabiwa kuwa watu 30,000. Pia wasemaji wa lugha jirani hujifunza Kibalantak kama lugha ya mawasiliano. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibalantak iko katika kundi la Kicelebiki.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibalantak kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.