Indonesia
Indonesia ni nchi ya visiwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Iko upande wa Kusini-Mashariki kati ya Bahari ya Uhindi na Pasifiki.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Bhinneka Tunggal Ika (Kijava/Kikawi: Umoja katika tofauti) Itikadi: Pancasila | |||||
Wimbo wa taifa: Indonesia Raya | |||||
Mji mkuu | Jakarta | ||||
Mji mkubwa nchini | Jakarta | ||||
Lugha rasmi | Kiindonesia | ||||
Serikali | Jamhuri Joko Widodo Ma'ruf Amin | ||||
Uhuru Kutangaza Kutambuliwa |
Kutoka Uholanzi 17 Agosti 1945 27 Desemba 1949 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,904,569 km² (16th) 4.85% | ||||
Idadi ya watu - 2015 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
255,461,700 (4th) 237,424,363 124.66/km² (84th) | ||||
Fedha | Rupiah (IDR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
various (UTC+7 to +9) not observed (UTC+7 to +9) | ||||
Intaneti TLD | .id | ||||
Kodi ya simu | +62
- |
Visiwa vyake ni sehemu ya Funguvisiwa la Malay, ingawa Guinea Mpya kwa kawaida haihesabiwi katika fungu hilo.
Indonesia imepakana na Papua Guinea Mpya kwenye kisiwa cha Guinea Mpya, pia na Timor ya Mashariki kwenye kisiwa cha Timor, halafu na Malaysia kwenye kisiwa cha Borneo.
Nchi nyingine zilizo karibu ni Australia, Singapur na Ufilipino.
Jiografia
haririIndonesia ni nchi ya visiwa 18,000 ilhali zaidi ya 6,000 kati ya hivyo vinakaliwa na watu.
Visiwa vikubwa vyenye wakazi wengi ni hasa vitano:
- Java
- Sumatra
- Kalimantan (Borneo ya Kiindonesia)
- Guinea Mpya (pamoja na nchi ya Papua Guinea Mpya)
- Sulawesi.
Historia
haririVisiwa vya Indonesia viliathiriwa na utamaduni wa Uhindi. Kisiasa kulikuwa na falme nyingi.
Tangu karne ya 17 Waholanzi walianza kujenga vituo na kueneza utawala wao. Waliita koloni lao "Uhindi wa Kiholanzi" ("Nederlands-Indië").
Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia Japani ikatwaa visiwa na kuwafukuza Waholanzi.
Mwisho wa vita kiongozi Sukarno akatangaza Indonesia kama nchi huru. Waholanzi walijaribu kurudisha utawala wao lakini walilazimishwa na Marekani kukubali uhuru wa nchi.
Wakazi, lugha, utamaduni, dini
haririNchi ina wakazi 270,203,917 (2020) hivyo ina nafasi ya nne kati ya mataifa makubwa duniani. Ni nchi yenye Waislamu wengi kuliko nyingine zote duniani. Makabila asili ni 300 hivi; kubwa zaidi ni Wajava (42 %).
Lugha rasmi ni Bahasa Indonesia (Kiindonesia) iliyoundwa katika karne ya 20 kama lugha ya taifa kutokana na lahaja ya Kimalay. Nchini kote kuna lugha za asili zaidi ya 700 (angalia orodha ya lugha za Indonesia). Jawa pia ina sanaa ya mwandiko wa kipekee maarufu kama mwandiko wa Batiki (Batik Tulus) unaochorwa kwa jora za nguo.[1]
Idadi kubwa ya wakazi (87.2 %) wanahesabiwa kuwa Waislamu (karibu wote Wasuni), 9.8 % kama Wakristo (Waprotestanti 6.9 %, Wakatoliki 2.9 %), 1.6 % kama Wahindu na 0.7 % kama Wabuddha. Wahindu wako hasa kwenye kisiwa cha Bali. Hizo zote ni dini zilizotambulika rasmi pamoja na ile ya Konfusio (0.05 %).
Picha
hariri-
National Museum of Indonesia, Central Jakarta
-
Wisma 46, jengo refu kuliko yote ya Indonesia, likiwa Jakarta
-
Jalan Thamrin, barabara muhimu zaidi ya Central Jakarta
-
Treni katika stesheni ya Gambir, Central Jakarta
-
Bung Karno Stadium inaweza kupokea watazamaji 100,000
-
Ramani ya Indonesia
-
Wilaya za Indonesia
-
Malioboro, barabara muhimu zaidi huko Yogyakarta
-
Trans Jogja Bus, mwendokasi wa Yogyakarta
-
Mapishi ya Kiindonesia: Soto Ayam (chicken soup), sate kerang (shellfish kebabs), telor pindang (preserved eggs), perkedel (fritter) na es teh manis (sweet iced tea)
-
An Indonesian Army infantryman participating in the U.N.'s Global Peacekeeping Operation Initiative
-
Pindad Panser "Anoa" shown during Indo Defense and Aerospace Expo 2008
-
B-25 Mitchell bombers of the AURI in the 1950s
-
GE U20C in Indonesia, #CC201-05
-
GE U20C "Full-Width Cabin" in Indonesia, #CC203-22
-
GE U20C full computer control locomotive in Indonesia, #CC204-06
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Batik S128. "Handwriting Batik (Batik Tulis) and Cities In Indonesia That Produce It". Toko Batik Online 2019. Iliwekwa mnamo 2019-05-11.
{{cite web}}
: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
Viungo vya nje
hariri- Serikali
- (Kiindonesia) (Kiingereza) Tovuti rasmi Archived 17 Februari 2012 at the Wayback Machine.
- Government of Indonesia Archived 17 Februari 2012 at the Wayback Machine.
- Minister of The State Secretary (Kiindonesia)
- Statistics Center
- Chief of State and Cabinet Members Archived 12 Oktoba 2014 at the Wayback Machine.
- Taarifa za jumla
- Indonesia entry at The World Factbook
- Indonesia Archived 26 Aprili 2009 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Indonesia katika Open Directory Project
- Indonesia profile from the BBC News
- Indonesia at Encyclopædia Britannica
- Wikimedia Atlas of Indonesia
- Official Site of Indonesian Tourism
- Key Development Forecasts for Indonesia from International Futures
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Indonesia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |