Shiza Kichuya
Mchezaji wa soka Tanzania
(Elekezwa kutoka Kichuya)
Shiza Ramadhan Kichuya, alizaliwa katika mkoa wa Morogoro (11 Desemba 1996), ni mchezaji wa soka katika timu ya Simba Sports Club. Baada ya kucheza Simba alisajiliwa nchini Misri.
Alianza maisha yake ya soka katika klabu ya watoto ya Champion ya mkoani Morogoro kabla ya kuhamia Moro Kids ya hapohapo mkoani Morogoro. Alicheza kwa mafanikio katika klabu hiyo.
Baadae alipata bahati ya kujiunga na klabu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro ambapo baada ya kuonesha kiwango kikubwa alisajiliwa na klabu ya Dar es salaam, Simba Sports Club. . Anacheza katika nafasi ya mshambuliaji na anatumia mguu wa kushoto.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shiza Kichuya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |