Mkoa wa Morogoro

Morogoro ni jina la mto, mji, wilaya na mkoa wa Tanzania.

Mnara wa saa,Morogoro
Mkoa wa Morogoro
Mahali pa Mkoa wa Morogoro katika Tanzania
Mahali pa Mkoa wa Morogoro katika Tanzania
Majiranukta: 8°0′S 37°0′E / 8°S 37°E / -8; 37
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Morogoro
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Dr. Stephen Kebwe
Eneo
 - Mkoa 73,039 km²
Idadi ya wakazi (2012)
 - 2,218,492
Tovuti: http://www.morogoro.go.tz/

Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 67000. Umepakana na mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Ruvuma, Iringa, Dodoma na Arusha.

Eneo lake ni km² 72 939, ambapo kuna wakazi 2,218,492 (mwaka 2012). Hivyo Morogoro ni kati ya mikoa mikubwa zaidi ya Tanzania.

UtawalaEdit

Mkoa ulikuwa na wilaya sita ambazo ndizo (idadi ya wakazi katika mabano): Kilosa (489,513), Kilombero (322,779), Morogoro Vijijini (263,920), Morogoro Mjini (228,863), Mvomero (260,525), Ulanga (194,209). Mwaka 2012 imeongezwa wilaya mpya ya Gairo na Wilaya ya Malinyi

Wakazi walio wengi hukalia wilaya za kaskazini. Robo yao huishi katika miji ya mkoa.

Ramani Wilaya au manisipaa Wakazi (2002) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Wilaya za Mkoa wa Morogoro
Wilaya ya Kilombero 321,611 5 19 81 14,918
Wilaya ya Kilosa 489,513 9 37 164 14,245
Wilaya ya Morogoro Vijijini 263,920 6 25 132 11,925
Wilaya ya Morogoro Mjini 227,921 1 19 - 531
Wilaya ya Mvomero 260,525 4 17 101 7,325
Wilaya ya Ulanga 193,280 5 24 65 24,560
Jumla 1,759,809 30 141 543 73,039
Makisio ya idadi ya watu kwa mwaka 2008 ni watu 2,021,714
kutokana na kiwango cha ongezeko la watu la asilimia 2.6 kwa mwaka.
Marejeo: Mkoa wa Morogoro

EneoEdit

Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani ya Bahari Hindi na Nyanda za Juu za Kusini Tanzania.

Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero, pia milima ya juu kama Uluguru yenye mlima wa Kimhandu wenye 2646 m juu ya UB.

Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndiyo mto wa kutoa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za wanyama za Mikumi na Udzungwa na sehemu ya eneo la kuwinda wanyama la Selous.

WakaziEdit

Kabila kubwa ni la Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru.

Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala, Wapogolo, Wandamba, Wabena, Wambungu, Wakutu na Wavidunda.

Upande wa dini, karibu nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo.

MawasilianoEdit

Barabara Kuu za lami za Dar es Salaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma hupita eneo la mkoa pamoja na reli ya kati Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Kilombero.

UchumiEdit

Matunda aina ya maembe yakiwa mtini huko Morogoro

Ardhi ya Morogoro ina takribani rutuba ya kufaa kwa mazao mengi. Lakini kilimo kinategemea hali ya mvua.

Karibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi.

Mazao ya sokoni hulimwa milimani.

Mkoa wa Morogoro ni eneo lililojaliwa na Mungu kwa uzalishaji wa sukari kwa wingi. Hasa Wilaya ya Kilombero ina mashamba makubwa ya miwa.

Hifadhi za mkoaEdit

Inabidi zitunzwe hifadhi mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wa Morogoro kwa sababu kutunzwa kwa hifadhi hizo kunaweza kukaleta faida mbalimbali kama vile: pesa za kigeni na pia maendeleo katika lugha mbalimbali.

Majimbo ya bungeEdit

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit