Kidudu-dubu
Kidudu-dubu | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Picha ya kidudu-dubu kwa hadubini ya elektroni
| ||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||
| ||||||
Ngazi za chini | ||||||
Ngeli, oda na familia
|
Vidudu-dubu (kutoka Kiholanzi beerdiertjes) ni viumbehai vinavyofanana na dubu wadogo sana wenye jozi nne za miguu; wengi zaidi wana mm 0.3-0.5 wakiwa wazima, lakini kuna spishi kadhaa za hadi mm 1.2 na nyingine za mm 0.1 tu. Wanatokea katika maji au mahali pa majimaji. Wanyama hawa wanaweza kuendelea kuishi katika hali za kuzidi kiasi: kutoka halijoto ya karibu na sifuri halisi hadi juu ya kiwango cha kuchemka, ukavu kabisa, kanieneo kubwa sana, ombwe kabisa na mnururisho kali unaoionisha. Wakikaa katika hali ya ukavu kabisa, hupoteza takriban maji yote mpaka kubaki na 3% tu na hata baada miaka kumi katika hali hii wanaweza kuamka na kuendelea kuishi.
Picha
hariri-
Kidudu-dubu upande wa kando
-
Kidudu-dubu upande wa chini
-
Kidudu-dubu akienda