Kielelezo
Kielelezo (pia: mfano au modeli kutoka Kiingereza mdel[1]) ni uwakilishi wa kina wa kitu, mtu au mfumo.
Modeli zinaweza kugawanywa katika modeli za kimwili (kama modeli ya meli au modeli ya mavazi) na modeli dhahania (mfano, seti ya milinganyo ya kihesabu inayoelezea jinsi angahewa linavyofanya kazi kwa madhumuni ya utabiri wa hali ya hewa). Modeli za dhahania au dhana ni muhimu sana katika falsafa ya sayansi.
Katika utafiti wa kitaaluma na sayansi inayotumika, modeli haipaswi kuchanganywa na nadharia: wakati modeli inalenga tu kuwakilisha uhalisia kwa madhumuni ya kuelewa au kutabiri ulimwengu vizuri zaidi, nadharia ina malengo makubwa zaidi kwa kudai kuwa ni maelezo ya uhalisia.
Tanbihi
haririViungo vya nje
hariri- media kuhusu Physical models pa Wikimedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kielelezo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |