Kifaduro
Kifaduro (au laringotrakeobronkitisi) ni hali ya upumuaji ambao husababishwa na maambukizi ya virusi kwa njia ya juu ya hewa. Maambukizi husababisha uvimbe ndani ya koo, ambao huharibu upumuaji wa kawaida na kuleta dalili za hali ya juu ya kikohozi cha kubweka, strida, na sauti iliyokauka. Inaweza kuleta dalili chache, kiasi, au kali zinazozidi zaidi usiku. Mara nyingi hutibiwa kwa dozi moja ya steroidi za kunywa; wakati mwingine epinephrini hutumika zaidi kwa visa kali. Ni nadra kulazwa hospitalini.
Croup | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Pulmonology, pediatrics |
ICD-10 | J05.0 |
ICD-9 | 464.4 |
DiseasesDB | 13233 |
MedlinePlus | 000959 |
eMedicine | ped/510 emerg/370radio/199 |
MeSH | D003440 |
Kifaduro hutambuliwa kwa kliniki, visababishi kali zaidi vya dalili vinapotengwa (yaani epiglotitisi au kitu kigeni katika njia ya hewa). Uchunguzi zaidi—kama vile vipimo vya damu, eksirei, na ukuzaji vimelea kwa kawaida huwa hahitajiki. Ni hali ya kawaida inayoathiri kiasi takriban asilimia 15 ya watoto kwa wakati fulani, kwa kawaida kati ya miezi 6 na miaka 5–6 ya umri. Huwa ni vigumu kupata kwa vijana na watu wazima. Wakati mwingine kwa sababu ya dondakoo, kisababishi hiki sasa ni cha umuhimu wa kihistoria katika Mataifa ya mashariki kwa sababu ya ufanisi wa chanjo, na kuboreshwa kwa usafi na viwango vya maisha.
Ishara na dalili
hariri
|
|
Problems listening to this file? See media help. |
Kifaduro huwa na sifa ya kikohozi cha 'kubweka, strida, sauti iliyokauka, na ugumu wa kupumua ambao kwa kawaida huwa mbaya zaidi usiku.[1] Kikohozi cha "kubweka" kwa kawaida huelezwa kuwa kinafanana na mlio wa seal au simba wa baharini.[2] Strida huzidishwa na kufadhaika au kulia, na iwapo unaweza kusikika wakati wa kupumzika, unaweza kuashiria uwembamba hatari kwa njia za hewa. Kifaduro inapokuwa zidi, strida inaweza kupungua sana.[1]
Dalili zingine ni pamoja na joto jingi mwilini, mafua (dalili za aina ya homa), na kuingia ndani kwa ukuta wa kifua.[1][3] Kudhoofika au kuonekana mgonjwa sana huashiria hali zingine za matibabu.[3]
Visababishi
haririKifaduro huchukuliwa kuwa kinasababishwa na maambukizi ya virusi.[1][4] Wengine hutumia jina hili kwa upana zaidi, kujumuisha laringotrakeobronkitisi kali, kifaduro cha spazimu, dondakoo ya zoloto, trakeitisi ya virusi, laringotrakeobronkitisi, na laringotrakeobronkoniumonitisi. Hali za kwanza mbili huhusisha maambukizi ya virusi na kwa kawaida huwa ndogo kwa kuzingatia simptomatolojia; nne za mwisho husababishwa na maambukizi ya bakteria na kwa kawaida huwa kali zaidi.[2]
Virusi
haririKifaduro cha virusi au laringotrakeitisi kali husababishwa na virusi vya parainfluenza, hasa aina 1 na 2, katika asilimia 75 ya visa.[5] Etiolojia zingine za virusi ni pamoja na influenza A na B, ukambi, virusi vya adeno na virusi vya sinksia ya kupumua (RSV).[2] Kifaduro cha spazimu husababishwa na aina sawa ya kikundi cha virusi kama laringotreikitisi kali, lakini haina dalili za maambukizi (kama vile joto jingi mwilini, vidonda vya koo,na ongezeko la seli nyeupe za damu).[2] Matibabu na matokeo ya matibabu pia huwa sawa.[5]
Bakteria
haririKifaduro cha bakteria kinaweza kugawanywa kuwa dondakoo la zoloto, trakeitisi ya bakteria, laringotrakeobronkitisi, na laringotracheobronkoniumonitisi.[2] Dondakoo la zoloto husababishwa na Corynebacterium diphtheriae ilhali trakeitisi ya bakteria, laringotrakeobronkoniumonitisi kwa kawaida husababishwa na maambukizi ya virusi vilivyo na uvimbe wa baadaye wa bakteria. Bakteria ya kawaida inayohusishwa ni Stafilokasi aureus, Streptokokasi niumoniae, Hemophilasi influenzae, na Moraxella catarrhalis.[2]
Pathofisiolojia
haririMaambukizi ya virusi yanayosababisha dondakoo husababisha kuvimba kwa larinksi, trakea, na bronki iliyo kubwa[4] kwa sababu ya kupenya kwa seli nyeupe za damu (hasa histiositi, limfositi, seli za plazma, na nutrofilisi).[2] Uvimbe husababisha kufungana kwa njia ya hewa ambapo, kunapoongezeka, husababisha ongezeko la tatizo la kupumua na upitaji wa hewa ulio na sifa ya kelele huitwao strida.[4]
Utambuzi
haririFeature | Number of points assigned for this feature | |||||
---|---|---|---|---|---|---|
0 | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 | |
Chest wall retraction |
None | Mild | Moderate | Severe | ||
Strida | None | With agitation |
At rest | |||
Sinosisi | None | With agitation |
At rest | |||
Kiwango cha ufahamu |
Normal | Disoriented | ||||
Air entry | Normal | Decreased | Markedly decreased |
Kifaduro ni utambuzi wa kliniki.[4] Njia ya kwanza ni kuwacha hali za vizuizi vingine kwa njia ya hewa iliyo juu, hasa epiglotitisi, njia ya hewa kifaa kigeni, stenosisi ya subglottic, anjioedema, jipu lililo nyuma ya farinksi, na trakeitisi ya bacteria.[2][4]
Eksirei ya upande wa mbele wa shingo haifanywi mara kwa mara,[4] ingawa itakapofanywa, inaweza kuonyesha jinsi trakea inavyokuwa nyembamba, iitwayo dalili ya steeple, kwa sababu ya stenosisi ya subglottic, iliyo sawa na steeple. Dalili ya steeple inashauriwa kufanyiwa utambuzi, lakini hukosekana katika nusu ya kila hali.[3]
Uchunguzi mwingine (kama vile upimaji wa damu na ukuzaji wa virusi) hazipendekezwi, kwa kuwa zinaweza kusababisha mfadhaiko usiofaa na hivyo kuongeza matatizo zaidi kwa njia ya hewa.[4] Wakati ukuzaji wa virusi uliopatikana kupitia pua na farinksi aspiresheni, inaweza kutumika kutambua kisababishi kikuu, kawaida hayajakubalishwa kwa mbinu za utafiti.[1] Maambukizi ya bakteria yanapaswa kuangaziwa ikiwa matibabu ya kawaida hayatafaulu, ambapo kiwango cha uchunguzi zaidi unaweza kuonekana.[2]
- Ukali
Mfumo unaotumika zaidi kwa kuainisha ukali wa kifaduro ni Westley score. Inatumika hasa kwa matumizi ya utafiti badala ya mazoezi ya kliniki.[2] Ni ujumla ya vidokezo vilivyotolewa kwa mambo matano: kiwango cha ufahamu, sainosisi, strida, kuingia, na kurudi kwa kwa hewa.[2] Vidokezo vya kila jambo vimetajwa kwa kila jedwali lililokulia, na alama ya mwisho iko katika kiwango cha 0 hadi 17.[6]
- Rekodi ya ≤ 2 kwa ujumla inaonyesha kifaduroisiyo kali. Kukohoa ulio na sauti wa kubweka na uliokauka unaweza kujitokeza, lakini hakuna strida wakati wa kupumzika.[5]
- Rekodi ya 3–5 kwa ujumla inaainishwa kama kifaduroisiyo kali. Hujitokeza na strida iliyosikika kwa urahisi, ingawa na dalili zingine kiasi.[5]
- Rekodi ya 6–11 kwa ujumla ni kifaduro iliyo kali. Hujitokeza na strida ya kawaida, lakini pia inaonyesha alama ya kuta ya kifua inapovutwa ndani.[5]
- Rekodi ya ≥ 12 kwa ujumla inaonyesha kukaribia kwa kushindwa kupumua. Kukohoa kwa sauti ya kubweka na strida inaweza kuwa sio maarufu katika kiwango hiki.[5]
Asilimia 85 ya watoto walio katika idara ya dharura wana ugonjwa usio mkali; kifaduro iliyo kali ni nadra (asilimia<1).[5]
Uzuiaji
haririHali nyingi za kifaduro zimezuiwa kwa chanjo ya influenza na dondakoo. Wakati moja, kifaduro inajulikana kama ugonjwa wa dondakoo, lakini na chanjo, sasa dondakoo ni nadra katika nchi zilizostawi.[2]
Matibabu
haririWatoto walio na kifaduro kwa ujumla huwekwa katika hali ya utulivu inavyowezekana.[4] Kawaida steroidi hutolewa, na epinefrini hutumika katika hali kali.[4] Watoto walio na uloweshaji wa oksijeni chini ya asilimia 92 wanapaswa kupata oksijeni,[2] na walio na kifaduro mkali wanaweza kulazwa kwa utathmini.[3] Iwapo oksijeni inahitajika, utoaji wa "kupitisha hewa" (kushikilia chanzo cha kutoa oksijeni kwa uso wa mtoto) inahitajika, kwa sababu inasababisha msukosuko ulio chini kuliko matumizi ya barakoa.[2] Kwa matibabu, chini ya asilimia 0.2 ya watu huhitaji upishaji neli kooni.[6]
Steroidi
haririKotikosteroidi, kama vile deksamethasoni na budesonidi, zimebainishwa kuwa zinaimarisha matokeo ya matibabu ya kifaduro zote kali kwa watoto.[7] Mgonjwa hutulia pakubwa kwa kipindi cha saa sita baada ya kupewa dawa hizi.[7] Huku dawa hizi zikiaminiwa kuwa bora zinapotumika kupitia kinywani, nje ya njia ya chakula, au kwa kuvutwa, njia ya kinywani hupendekezwa.[4] Kipimo kimoja tu cha dawa ndicho kinachohitajika, na huaminiwa kuwa salama.[4] Kipimo cha miligramu/kilogramu 0.15, 0.3 na 0.6 cha deksamethasoni umebainishwa kuwa bora.[8]
Epinefrini
haririHali ya kifaduro cha kiwango wastani hadi kiwango kali inaweza kutulizwa kwa muda tu kwa kutumia epinefrini ya kupulizwa.[4] Huku epinefrini ikituliza ukali wa kifaduro kwa muda wa dakika 10–30, manufaa yake hudumu kwa takriban saa 2 tu.[1][4] Ikiwa hali hii itatulia kwa muda wa saa 2–4 baada ya matibabu huku ikiwa hakuna mzuko wa matatizo yoyote, mtoto huachiliwa hospitalini.[1][4]
Matibabu mengine
haririHuku matibabu mengine ya kifaduro yakiwa yametafitiwa, hakuna yoyote yaliyo na dhihirisho ya kutosha ili yatumike. Kuvuta mvuke au hewa yenye maji ni njia ya kitamaduni ya kujitibu, lakini utafiti wa kimatibabu haujatibithisha ubora wake[2][4] ni nadra kwa sasa.[9] Matumizi ya dawa za kikohozi, ambazo kwa kawaida zina dextromethorphan na/au guiafenesin, pia inakataliwa.[1] Huku vutaji wa heliox (mchanganyiko wa heliamu na oksijeni) ili kupunguza utendakazi wa upumuaji ulitumika mbeleni, lakini hakuna tibitisho la kutosha kupendekeza matumizi yake.[10] Kwa sababu kifaduro ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi, antibiotiki haitumiki japo tu maambukizi ya pili ya bakteri yanaposhukiwa. [1] Kwa visa ambavyo vina maambukizi ya pili ya bakteria, antibiotiki aina ya vancomycin na cefotaxime inapendekezwa.[2] kwa visa vikali vinavyohusisha influenza A au B, dhidi ya virusivizuio vya niuraminidesi inaweza kutumika.[2]
Prognosisi
haririKwa kawaida kifaduro inayosababishwa na virusi unaopotea kivyake, lakini ni nadra isababishe kifo kufuatia kushindwa kupumua na/au mshtuko wa moyo.[1] Dalili za hali hii hupotea kwa kipindi cha siku mbili, laikini zinaweza kudumu kwa hadi siku saba.[5] Matatizo mengine ambayo ni nadra kutokea ni pamoja na uvimbe wa bomba la pumzi, nimonia, na uvimbe wa mapafu.[5]
Epidemiolojia
haririKifaduro huathiri takriban asilimia 15 ya watoto, na hutokea katika umri kati ya miezi 6 na miaka 5-6.[2][4] hali hii huchukua asilimia 5 ya takwimu za wagonjwa wote wa umri huu wanaolazwa hospitalini.[5] Kwa visa nadra hali hii inaweza kutokea kwa wototo wachanga kama umri wa miezi 3 na kwa wototo wakubwa hadi umri wa miaka 15.[5] Watoto wa kiume huathirwa kwa zaidi ya asilimia 50 mara kwa mara kuliko wa kike, na kuna ongezeko la maenezi ya hali hii katika majira ya kupukutika kwa majani.[2]
Historia
haririNeno kifaduro hutokea kwa lugha ya zamani ya Kingereza kitenzi kifaduro, kumaanisha "kulia kwa sauti iliyokauka"; jina hili lilitumika kwa ugonjwa huu kwa mara ya kwanza nchini Scotland kisha kuenezwa katika karne ya 18.[11] Kifaduro inayohusisha dondakoo kimejulikana tangu enzi za Homer Kale za Ugiriki na hadi 1826 ambapo kifaduro ya virusi ilitafautishwa kutoka kifaduro kwa sababu ya dondakoo na Bretonneau.[12] Kuanzia hapo kifaduro ya virusi ikaitwa "kifaduro ya kijamba" na Mfaransa, na kisha "kifaduro" ikajulikana kama ugonjwa unaosababishwa na bakteria ya dondakoo.[9] Kifaduro inayosababishwa na dondakoo inakaribia kusahaulika kufuatia kuzinduliwa kwa chanjo bora.[12]
Marejeo
hariri- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 Rajapaksa S, Starr M (2010). "Croup – assessment and management". Aust Fam Physician. 39 (5): 280–2. PMID 20485713.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 2.14 2.15 2.16 2.17 2.18 Cherry JD (2008). "Clinical practice. Kifaduro". N. Engl. J. Med. 358 (4): 384–91. doi:10.1056/NEJMcp072022. PMID 18216359.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 "Diagnosis and Management of Croup" (PDF). BC Children’s Hospital Division of Pediatric Emergency Medicine Clinical Practice Guidelines.
- ↑ 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 4.11 4.12 4.13 4.14 4.15 Everard ML (2009). "Acute bronchiolitis and croup". Pediatr. J. CL. North Am. 56 (1): 119–33, x–xi. doi:10.1016/j.pcl.2008.10.007. PMID 19135584.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ 5.00 5.01 5.02 5.03 5.04 5.05 5.06 5.07 5.08 5.09 5.10 5.11 Johnson D (2009). "Croup". Clin Evid (Online). 2009. PMC 2907784. PMID 19445760.
- ↑ 6.0 6.1 6.2 Klassen TP (1999). "Croup. A current perspective". Pediatr. Clin. North Am. 46 (6): 1167–78. doi:10.1016/S0031-3955(05)70180-2. PMID 10629679.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ 7.0 7.1 Russell KF, Liang Y, O'Gorman K, Johnson DW, Klassen TP (2011). "Glucocorticoids for croup". Cochrane Database Syst Rev. 1 (1): CD001955. doi:10.1002/14651858.CD001955.pub3. PMID 21249651.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Port C (2009). "Towards evidence based emergency medicine: best BETs from the Manchester Royal Infirmary. BET 4. Dose of dexamethasone in croup". Emerg Med J. 26 (4): 291–2. doi:10.1136/emj.2009.072090. PMID 19307398.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ 9.0 9.1 Marchessault V (2001). "Historical review of croup". Can J Infect Dis. 12 (6): 337–9. PMC 2094841. PMID 18159359.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ Vorwerk C, Coats T (2010). "Heliox for croup in children". Cochrane Database Syst Rev. 2 (2): CD006822. doi:10.1002/14651858.CD006822.pub2. PMID 20166089.
- ↑ Online Etymological Dictionary,[1] Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.. Accessed 2010-09-13.
- ↑ 12.0 12.1 Feigin, Ralph D. (2004). Textbook of pediatric infectious diseases. Philadelphia: Saunders. uk. 252. ISBN 0-7216-9329-6.