Homeri (pia: Homer; kwa Kigiriki: Ὅμηρος homeros) ni jina la mshairi mashuhuri kabisa wa Ugiriki ya Kale. Mashairi makubwa yanayosimulia vita vya Troya (Ilias) na misafara ya mfalme Odiseo (Utenzi wa Odisei) yamehifadhiwa kama kazi zake.

Sanamu hii ya Homer inapatkana katika makumbusho ya Kiingereza London; ni mwigo wa Kiroma wa mfano wa Kigiriki
Homer (William Bouguereau, 1874)

Maswali juu yakeEdit

Wataalamu wa leo hutofautiana kama Homeri alikuwa kweli mtunzi wa mashairi hayo au kama ni sehemu za mashairi haya tu yaliyotungwa naye wakiamini ya kwamba kwa jumla ni mashairi ya kale yaliyowahi kuimbwa kabla yake. Pia kuna wataalamu wanaouliza kama Homeri alikuwa mtu wa kihistoria au kama ni jina tu lililopachikwa kwa mashairi haya.

MaishaEdit

Kufuatana na mapokeo ya kale Homeri alikuwa mshairi kipofu aliyeishi katika eneo la Ionia (Asia Ndogo) lililokaliwa na walowezi Wagiriki mnamo karne ya 8 KK. Miji mbalimbali ya Ionia hutajwa kama mahali pa kuzaliwa kwake. Jina la mama yake lilikuwa Kreitheïs. Anasemekana alikufa kwenye kisiwa cha Ios.

KujisomeaEdit

Matoleo ya kazi yakeEdit

Kwa Kigiriki

Tafsiri ya mstari-kwa-mstariEdit

Tafsiri kadhaa kwa KiingerezaEdit

Kuhusu HomerEdit

Maandiko muhimu juu ya HomerEdit

Maelezo ya maandiko yakeEdit

Kuhusu tarehe za mashairi yakeEdit

  • Janko, Richard (1982). Homer, Hesiod and the Hymns: Diachronic Development in Epic Diction, Cambridge Classical Studies. Cambridge: Cambridge University Press. 

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.