Kikuche
Kikuche utosi-mweusi
Kikuche utosi-mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Malaconotidae (Ndege walio na mnasaba na mbweta)
Jenasi: Bocagia Shelley, 1894

Tchagra Lesson, 1831

Spishi: B. minuta (Hartlaub, 1858)

T. anchietae (Barboza du Bodage, 1896)
T. australis (A. Smith, 1836)
T. jamesi (Shelley, 1885)
T. senegalus (Linnaeus, 1766)
T. tchagra (Vieillot, 1816)

Vikuche ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Bocagia na Tchagra katika familia Malaconotidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Ndege hawa wana rangi ya kijivu mgongoni, rangi ya kahawiachekundu mbawani na rangi ya kijivu au nyeupe chini; mlia mweusi unapitia macho. Wana domo nene lenye ncha kwa kulabu. Hula wadudu wakubwa hasa na vertebrata wadogo pia, kama vyura, mijusi na nyoka wadogo. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini au kichakani na jike huyataga mayai 2-3.

Spishi

hariri