Kitabu cha Kilwa

(Elekezwa kutoka Kilwa Chronicle)

Kitabu cha Kilwa (kwa Kiingereza: Kilwa Chronicle) ni maandishi ambayo yanaaminika kujikita katika masimulizi na mapokeo ya mdomo, ambayo yanaonyesha historia halisi ya miji ya Waswahili ya Kilwa, katika visiwa vya bahari ya Hindi vilivyo karibu na pwani ya Afrika ya Mashariki.

Inasimulia nasaba ya masultani wa Kilwa, ikifuata kugunduliwa kwa mji na Waajemi kutoka Shirazi na Hormuz kwenye karne ya 10 mpaka kufika kwa Wareno kwenye karne ya 16. Uchunguzi wa DNA za zamani unaonyesha na kukubali kwa kiasi kikubwa kuwa masimulizi hayo ni ya kweli.

Kuna vyanzo viwili vya kitabu hicho: Kitāb al-Sulwa kwa Kiarabu na tafsiri yake ya Kireno ambayo ni sehemu ya kitabu Décadas da Ásia kilichoandikwa na mwanahistoria João de Barros. [1]

Vyanzo

hariri
  • João de Barros (1552) Décadas da Ásia: Dos feitos, que os Portuguezes fizeram no descubrimento, e conquista, dos mares, e terras do Oriente., Dec. I, Lib. 8, Cap. 6 (p. 223ff)
  • Strong, S. Arthur (1895) "The History of Kilwa, edited from an Arabic MS", Journal of the Royal Asiatic Society, January (No volume number), pp. 385–431. online

Marejeo

hariri
  1. Delmas, Adrien (2017). "Writing in Africa: The Kilwa Chronicle and other Sixteenth-Century Portuguese Testimonies". Katika Brigaglia, Andrea; Nobili, Mauro (whr.). The Arts and Crafts of Literacy: Islamic Manuscript Cultures in Sub-Saharan Africa. Berlin, Boston: De Gruyter. uk. 189. ISBN 9783110541441. OCLC 1075040220.