Kilwa Kisiwani
Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa
Kilwa Kisiwani | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Lindi |
Wilaya |
Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko katika Mkoa wa Lindi, Tanzania.
Ndipo mahali pa mji wa Kilwa ya kihistoria iliyokuwa mji mkubwa kabisa kati ya miji ya Waswahili katika pwani ya Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya 14 hadi karne ya 16 BK.
Mji muhimu zaidi wa Uswahilini
Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa kituo muhimu cha biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 Kilwa ikawa muhimu kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.
Katika karne ya 14 - kati ya 1330 na 1340 BK - mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya kwanza ya kimaandishi kuhusu mji huo.
Majengo makubwa yalijengwa yakiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama vile msikiti mkuu, Jumba ya kifalme ya Husuni Kubwa, Boma la Kireno Kilwa na mengine mengi.
Kuja kwa Wareno
Kuja kwa Wareno katika karne ya 16 ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne ya 18 na ya 19 ikapata upya nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Mwisho wa biashara hiyo ulimaliza utajiri wa Kilwa.
Kilwa leo
Leo hii Kilwa Kisiwani ipo katika eneo la Tanzania lisilotembelewa kwa urahisi.
Hata hivyo kisiwa ni kati ya Hifadhi za kiutamaduni muhimu sana, hata imeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).
Katika wilaya hiyo kuna mahali pengine pa urithi wa dunia, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
- Chittick, H. Neville (1974), Kilwa: an Islamic trading city on the East African coast (2 Vols), Nairobi: British Institute in Eastern Africa. Volume 1: History and archaeology; Volume 2: The finds.
- Dunn, Ross E. (2005), The Adventures of Ibn Battuta, University of California Press, ISBN 0-520-24385-4. First published in 1986, ISBN 0-520-05771-6.
- João de Barros (1552) Décadas da Ásia: Dos feitos, que os Portuguezes fizeram no descubrimento, e conquista, dos mares, e terras do Oriente., Dec. I, Lib. 8, Cap. 6 (p. 223ff)
- Strong, S. Arthur (1895) "The History of Kilwa, edited from an Arabic MS", Journal of the Royal Asiatic Society, January (No volume number), pp. 385–431. online
Viungo vya nje
- Kilwa katika Historia ya Waswahili (BBC)
- Kilwa Kisiwani Site Page from the Aluka Digital Library
- World Monuments Fund Project Page for Kilwa
- Free resource for tourists on Kilwa Archived 4 Desemba 2021 at the Wayback Machine.
- Geonames.org
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kilwa Kisiwani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |