Kingoyo

Kingoyo
Kingoyo utosi-mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Pelecaniformes (Ndege kama makorongo)
Familia: Ardeidae (Ndege walio na mnasaba na koikoi)
Leach, 1820
Ngazi za chini

Jenasi 5:

Vingoyo ni ndege wakubwa wa jenasi mbalimbali za familia Ardeidae wenye domo refu na nyembamba lakini miguu mifupi kuliko spishi nyingine za familia hii. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Spishi moja huitwa ngojamalika. Ndege hawa wana rangi nyeupe na nyeusi, nyekundu au ya manjano. Vingoyo hula samaki hasa. Hizi ni spishi zinazojificha ndani ya uoto. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti au matete. Hata matago yamefichika kwa kawaida.

Spishi za AfrikaEdit

Spishi za mabara mengineEdit

Spishi za kabla ya historiaEdit

  • Nycticorax fidens (MMA, mwisho wa Miocene)
  • Nycticorax kalavikai (Niue Night Heron) (Niue)
  • Nycticorax sp. (‘Eua Night Heron) (Tonga)
  • Nycticorax sp. (Lifuka Night Heron) (Tonga) - labda ni moja na spishi ya ‘Eua
  • Nycticorax sp. (Faiyum, Misri, mwanzo wa Oligocene)

PichaEdit