Kipazasauti (pia spika) ni kifaa kinachotoa sauti kwenye redio, runinga au ala za muziki wa elektroniki. Kifaa hiki kina uwezo wa kupaza sauti asilia na hapo ndipo asili ya jina lake.

Kipaza sauti: Mwendo wa sumaku (nyekundu) unasababisha mitetemo ya utando ndani yake (A) inayoendelea kama mitetemo ya hewa nje yake (B) inayofika kwenye sikio kama sauti
Kipaza sauti ya kawaida yenye utando wa karatasi ngumu

Misingi ya kipazasauti

hariri

Inapokea mishtuko ya umeme na kuibadilisha kuwa mwendo wa sumaku ndogo ndani yake inayosogea mbele na nyuma. Sumaku inaunganishwa na mtando wa kipaza sauti na kuitetemesha kwa miendo yake. Mitetemo ya utando ndani ya kipaza sauti inaendelea kama mitetemo ya hewa mbele ya utando. Mitetemo inasambaa na kupokelewa na kiwambo cha sikio kama sauti. Sauti inayotoka kwa kipazasauti yategemea sauti ya anayeongea na kinasasauti (microphone) inayopokea mitetemo ya sauti kwa utando ndani yake. kuibadilisha kuwa mishtuko ya umeme inayoweza kupokewa tena na kipazasauti.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.