Kipembezo
Katika utarakilishi, kipembezo (pia: pembezo[1]; kwa Kiingereza: peripheral) ni kitumi chote cha tarakilishi ambacho kinatumika ili kuingia na kuondoa taarifa kutoka tarakilishi.
Kuna aina kadhaa za vipembezo.
- Kitumi cha kuingia ambacho kinatuma data tarakilishi, kama kipanya, baobonye, kamera pembuzi au kitambazo.
- Kitumi cha kutolea ambacho kinatoa kitoleo cha tarakilishi, kama kichapishi, kiwambo au kipaza sauti.
TanbihiEdit
- ↑ ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY (INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.). kamusi.kiswahilipedia.org. Iliwekwa mnamo 2020-11-24.
MarejeoEdit
- Kiputiputi, O. (2011). Kamusi sanifu ya kompyuta. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, K.602.