Kibodi
Kibodi (pia: Kiibodi[1], Kicharazio[2], Baobonye au Bodidota/Bodi ya dota[3]; kwa Kiingereza: keyboard) ni kifaa muhimu kinachomwezesha mtu kuweka maandishi na namba kwa tarakishi (kompyuta). Inafanywa na vibonye vingi kwa ajili ya kila herufi na alama nyingine zinazotumiwa mara kwa mara.

Kibodi ni pia sehemu ya chombo cha muziki k.v. piano, iliyo na vibonye vyenye rangi vinavyobonyezwa ili kutoa sauti.
Kwa tarakilishi nyingi ni kifaa kikuu cha kuingizia habari mashineni.
Kuna mifumo mbalimbali za baobonye kulingana na lugha.
Muundo wa kawaida kwa lugha zinazotumia alfabeti ya Kilatini ni QWERTY (hizi ni herufi 6 za kwanza).
Muundo huu unaweza kuchosha mikono na vidole. Ulianzishwa zamani za mashine za kupiga chapa na mfumo wa herufi ulilenga kutovurugisha mikono ya taipu. Siku hizi ni kama hakuna taipu tena, lakini watu waliozoea muundo umebaki vile.
Majina ya vibonyezo (keys) hariri
- kibonyezo (cha) kibadalishi ‘alt(ernate) key’
- kibonyezo (cha) kirejeshi ‘back space’
- kibonyezo (cha) kiepushi ‘escape key’
- kibonyezo (cha) kuendelea ‘enter key’
- kibonyezo (cha) herufi kubwa ‘caps lock’
- kibonyezo (cha) huduma ‘function key’
- kibonyezo (cha) ingizo ‘insert key’
- kibonyezo (cha) kudhibiti ‘control key’
- kibonyezo (cha) kufutia ‘delete key’
- kibonyezo (cha) mahesabu ‘numeral key’
- kibonyezo (cha) mpangilio ‘tab key’
- kibonyezo (cha) nafasi ‘space bar’
- kibonyezo (cha) nyumbani ‘home key'
- kibonyezo (cha) kuhama ‘shift key’
- kibonyezo (cha) ukurasa unaofuata ‘page down key’
- Kibonyezo cha ukurasa uliotangulia ‘page up key’
Tazama pia hariri
Marejeo hariri
- ↑ KKS Kamusi Kuu ya Kiswahili, toleo la nne, TUKI 2019
- ↑ Kamusi Kuu ya Kiswahili
- ↑ Kamusi ya Karne ya 21, EMAC, BAKITA na KIE. ISBN: 998-702-097-6