Kitororo
Kitororo Paji-jekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Piciformes (Ndege kama vigong'ota)
Familia: Lybiidae (Ndege walio na mnasaba na zuwakulu)
Jenasi: Pogoniulus
Lafresnaye, 1842

Vitororo au kongogolo ni ndege wadogo wa jenasi Pogoniulus katika familia Lybiidae. Ndege hawa ni matoleo madogo ya zuwakulu na mwenendo wao ni takriban sawa na hawa. Vitororo ni ndege wadogo wenye 9-12 cm na 7-15 g. Wana rangi ya kijivu, nyeusi au majani, mistari myeupe na madoa mekundu au njano. Hula wadudu na beri, matini madogo na beri za spishi za kirukia hasa. Dume na jike pamoja huchimba tundu katika tawi au shina lililooza na jike huyataga mayai 2-4 ndani yake.

Spishi

hariri