Kitotela ni lugha ya Kibantu nchini Zambia na Namibia inayozungumzwa na Watotela. Idadi ya wasemaji imepungua sana. Mwaka wa 1971 idadi ya wasemaji wa Kitotela nchini Zambia ilikuwa watu 14,000, lakini katika sensa ya mwaka wa 2010 wamebaki wasemaji 1120 tu. Idadi ya wasemaji nchini Namibia ni 100 tu (2006). Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kitotela iko katika kundi la K40.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitotela kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.