Vivumishi vya kuonesha
(Elekezwa kutoka Kivumishi cha kuonesha)
Mifano |
---|
|
Vivumishi vya kuonesha (pia: "vivumishi vya kuashiria") ni maneno yanayotoa taarifa ihusuyo nomino au kiwakilishi cha nomino kwa kudokeza umbali au ukaribu wa nomino hiyo iliyotajwa kutoka kwa mzungumzaji. Umbali huo unaweza kuwa karibu, mbali kidogo, au mbali sana. Pia tunaweza kuvitupia katika wingi na umoja tukizingatia ngeli za nomino na upatanisho wa kisarufi.
- Mifano
- Kibuyu kile kina maziwa
- Jembe hili ni mali yangu
- Gari hilo limepata ajali
- Kitabu hiki ni kizuri
- Mambo haya siyawezi
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vivumishi vya kuonesha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |