Kiwakilishi nafsi
Mifano |
---|
*Maneno kama -ake, -ako, -angu, -ao na -etu huitwa viwakilishi/kiwakilishi vimilikishi/kimilikishi. |
Kiwakilishi nafsi (pia: Kiwakilishi cha nafsi) ni aina ya neno/maneno yanayosimama badala ya majina yanayotaja nafsi za watu. Viwakilishi vya nafsi hugawanyika katika makundi mawili, nayo ni:
- Viwakilishi vya nafsi huru
- Viwakilishi vya nafsi kiambata
Mchanganuo
haririViwakilishi vya nafsi huru
haririHaya ni maneno mazima yanayoweza kusimama peke yake bila kuambatanishwa katika neno au mzizi wa neno jingine.
Nafsi | Umoja | Wingi |
---|---|---|
I | Mimi | Sisi |
II | Wewe | Ninyi/nyinyi |
III | Yeye | Wao |
- Mifano zaidi
- Mimi ni mwalimu
- Sisi ni walimu
- Wewe ni mwalimu
- Nyinyi ni walimu
- Yeye ni mwalimu
- Wao ni walimu
Viwakilishi vya nafsi kiambata
haririHizi ni mofimu tegemezi/vipande vya maneno vinavyoambikwa/vinavyoambatanishwa katika neno au mzizi wa neno jingine ili kudokeza nafsi inayohusika. Mfano: Nikija nitawapeleka, Tukisoma tutafaulu, Ukija utakiona cha moto, Mkija atawaona, Asiyekujua hakuthamini, Waliosafiri wamefika salama.
Nafsi | Umoja | Wingi | Mzizi |
---|---|---|---|
I | Ni | Tu | Nikija/Tukija |
II | U | M | Ukija/Mkija |
III | A | Wa | Akija/Wakija |
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- Massamba, David. 2004. "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiwakilishi nafsi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |