Kiwanda cha kusafisha mafuta

Kiwanda cha kusafisha mafuta (kwa Kiing. oil refinery, petroleum refinery) ni kiwanda ambapo mafuta ghafi hutumiwa kuzalisha bidhaa za mafuta kama vile petroli, diseli, lami au gesi ya mafuta ya petroli (LPG) kwa njia ya ukenekaji kisehemu. [1] [2]

Kiwanda cha Kusafisha cha Anacortes ( Tesoro ), upande wa kaskazini wa Machi Point kusini mashariki mwa Anacortes, Washington .

Kimsingi mafuta ghafi huchemshwa na kemikali tofauti ndani yake ambazo hutenganishwa na kusafishwa kila moja peke yake. Maana mafuta ghafi kikemia ni mchanganyiko wa dutu nyingi na kila moja inachemka na kuyeyuka kwa halijoto tofauti ambapo inajitenga na nyingine. Mvuke wa sehemu hizo tofauti unapozwa na kuwa miminika baadaye, isipokuwa sehemu hizo ambazo zinabaki kama gesi.

Marejeo

hariri
  1. Gary, J.H. and Handwerk, G.E (1984). Petroleum Refining Technology and Economics (tol. la 2nd). Marcel Dekker, Inc. ISBN 0-8247-7150-8.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  2. Leffler, W.L. (1985). Petroleum refining for the nontechnical person (tol. la 2nd). PennWell Books. ISBN 0-87814-280-0.

Viungo vya Nje

hariri