Koili Devi Mathema

Koili Devi Mathema (1929 - 2007) alikuwa mwanamke wa kwanza aliyekuwa mwimbaji na mtunzi katika tasnia ya muziki nchini Nepal.

Hufahamika pia kama 'Cuckoo bird', jina ambalo linatokana na maana ya jina lake 'Koili' katika lugha ya Kinepali. Anajulikana kwa sauti yake ya kipekee kama ilivyo ya ndege anayeitwa Cuckoo.

Kwa msaada wa shangazi yake, aliingia katika jumba la kifalme la Singh Sumsher JBR akiwa na umri wa miaka 11, akiwa msaidizi. Koili Devi ni jina lililompa mafanikio na umaarufu. Alianza kuimba na kucheza katika bendi ya Singha Durbar. Mnamo mwaka 2007 baada ya kuanzishwa kwa demokrasia nchini, akawa mwimbaji huru katika Radio ya Nepal. Anatokea kwenye kizazi cha kwanza cha waimbaji wa Nepal ambao ni waimbaji wenye ujuzi. Nyimbo zake pia zimekuwa zikitumika katika filamu mbalimbali.[1][2][3]

Marejeo hariri

  1. "Personality Of the Week: Koili Devi Mathema". Nepali Radio Texas. 18 January 2012. Iliwekwa mnamo 11 December 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Singing legend Koili Devi dies at 78". The Himalayan. 22 December 2007. Iliwekwa mnamo 11 December 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "Koili Devi, singer with the cuckoo voice". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-06. Iliwekwa mnamo 6 December 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Koili Devi Mathema kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.