Kombolela ni mchezo asilia wa watoto wa Afrika Mashariki.

Mchezo huu unashirikisha watoto watano na kuendelea. Hao wanatawanyika kwenda kujificha. Mmoja anashika doria kulinda kopo au mpira huku akiangaza macho kutafuta waliojificha.

Baada ya kuona wenzake kadhaa, ikitokea kwamba mmoja ambaye hajaonekana analipiga kopo anakuwa ameokoa walioonekana. Hivyo mlinzi huendelea hadi atakapowaona wote. Wa kwanza kuonekana ndiye anayefuatia kulinda.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kombolela kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.