Kompyuta bapa
Kompyuta bapa, ni kifaa kinachoweza kubebeka, kwa kawaida ina mfumo wa uendeshaji wa simu na LCD ya ushughulikiaji kwa kugusa kioo chake, ina betri inayoweza kuimarishwa nguvu yake kila inapokuwa imekwisha.
Kompyuta bapa, hufanya kile ambacho kompyuta za kawaida zinafanya, lakini hazina uwezo wa I/O ambao kompyuta za kawaida zinazo.
Kompyuta bapa za kisasa zinafanana na simu za kisasa, tofauti tu ni kuwa kompyuta bapa ni kubwa zaidi kuliko simu za mkononi, na skrini ya inchi 7 na sm 18 kama ikipimwa kwa mshazari.