Nguvu
Nguvu ni uwezo wa kusababisha jambo fulani.
Kwa mfano,
- katika kiumbehai ni uwezo wa kosogea, kuinua vitu n.k.
- katika jinsia mara nyingi ni sifa inayopatikana zaidi katika ile ya kiume kuliko ile ya kike
- katika siasa ni mamlaka ya kuamua na kuagiza
- katika fizikia ni msukumo au mgongano wa vitu ambao unatoa nishati na unaitwa kani
- katika uchumi ni rasilimali au fedha za mtu
- katika elimu jamii ni tunda la mshikamano wa watu au taasisi
- katika maadili ni mojawapo ya maadili bawaba
- katika dini ni hasa uweza wa Mungu ambao unasisitizwa kwa kumuita Mwenyezi Mungu, yaani Mweza yote.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |