Open main menu

Kulala kwa Mama wa Mungu

Picha takatifu ya fumbo hilo iliyochorwa na msanii wa Novgorod, Urusi.

Kulala kwa Mama wa Mungu ni sikukuu ya Kanisa ambayo ni maarufu katika Ukristo wa mashariki, yaani Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Makanisa Katoliki ya Mashariki vilevile.

Inaadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Agosti baada ya wiki mbili za mfungo.

Inalingana na sherehe ya Maria kupalizwa mbinguni inayofanywa na Kanisa la magharibi siku hiyohiyo.

Neno "kulala" linachukuliwa kwa maana ya "kufa" kabla ya "kufufuliwa" na "kuchukuliwa mbinguni" kwa mwili wake.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit