Ukristo wa Mashariki

(Elekezwa kutoka Ukristo wa mashariki)

Ukristo wa Mashariki ni jina linalojumlisha madhehebu yote ya Ukristo yaliyotokea upande wa mashariki wa Bahari ya Kati na nje ya Dola la Roma yakiwa na mielekeo tofauti na ile ya Kanisa la Magharibi, ambalo ndilo aina ya Ukristo iliyoenea zaidi duniani pamoja na ustaarabu wa magharibi ulioathiriwa nayo.

Kristo Pantocrator, sehemu ya Deesis katika Hagia Sophia - Konstantinopoli (Istanbul) karne ya 12.

Unajumlisha hasa makanisa ya Waorthodoksi wa Mashariki na Waorthodoksi, ambayo yalitengana na Kanisa la Magharibi hasa katika karne ya 5 na karne ya 11, lakini pia Makanisa Katoliki ya Mashariki ambayo yana ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.

Makanisa hayo yanatofautiana sana kwa sababu toka mwanzo yalizingatia utamadunisho wa imani katika jamii husika. Hata hivyo yana sifa nyingi za pamoja katika teolojia, liturujia, maisha ya Kiroho, sheria n.k.

Kwa sasa wanajumuisha waamini milioni 300 hivi duniani kote.

Yale makubwa zaidi ni Kanisa la Kiorthodoksi la Kirusi na Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia.

Matawi ya Ukristo yalivyotokea katika historia ya Kanisa. Upande wa juu ndio Kanisa la Magharibi, upande wa chini Makanisa ya Mashariki. Unene wa mistari haulingani na ukubwa wa madhehebu husika.


Marejeo Edit

Viungo vya nje Edit

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukristo wa Mashariki kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.